Walimu watakiwa kuepuka habari potofu za uundwaji wa mfuko
mmoja wa jamii.
Walimu wametakiwa
kuondokana na dhana potofu kuwa uundwaji kuwa mfuko wa
jamii mmoja utawapunja mafao yao baada ya kustaafu inayowasababisha
kuomba kustaafu kwa hiari.
Hatua hiyo imekuja baada ya wimbi kubwa la walimu kuomba kustaafu kwa hiari kutokana na habari za uongo
za mitandaoni zinazoeleza endapo utaundwa mfuko huo mafao yao yatapunjwa.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Tume ya Utumishi wa Walimu Tanzania,
Winfrida Rutahindwa katika Mkutano uliowakutanisha Maofisa elimu, walimu na Wakuu wa Shule za Manispaa ya
Ilala.
Amesema idadi kubwa ya walimu wamekuwa wakiomba kustaafu
sababu ya habari za uongo zinazosambazwa na kwamba mfuko huo utakapoundwa
utawasaidia kuwaborshea maslahi ya mafao yao.
“Wimbi kubwa la walimu wanastaafu kwa hiari kuogopa kupunjwa
mafao kisa mchakato wa kuundwa mfuko mmoja wa jamii nawaombeni muwe na subira
serikali inafanya jambo jema la
kuwanufaisha,”amesema.
Amewataka walimu kutekeleza majukumu yao kwa kufuata sheria
na taratibu za utumishi wa umma na kwamba kufanya hivyo kutasaidia kuongeza
ufaulu wa wanafunzi.
Amewasisitiza maofisa elimu na wakurugenzi kuwahudumia
vizuri pale wanapowasilisha changamoto zao na kwamba kuwanyanyasa kutasababisha
matokeo mabaya ya wanafunzi.
Amewakumbusha wakuu wa vyuo nchini kutopokea walimu ambao
hawajawasilisha barua za ruhusa ya masomo
na kuwataka walimu kufundisha kwa bidii..
Comments