Mshindi wa BBA mwaka 2013 kutoka Namibia, (The Chase) Dillish Mathews baada ya kudaiwa kuwa kwenye mahusiano na mwanasoka wa Togo na klabu ya Istanbul BaÅŸakÅŸehir, Emmanuel Adebayor – Wawili hao wamedaiwa kumwagana.
Dillish na Adebayor waliingia kwenye vichwa vya habari vya kuwa wapenzi tangu mwishoni mwa mwaka jana.
Habari za mahusiano ya wawili hao kuvunjia zilianzia kwenye ujumbe ambao Dillish aliuweka kwenye mtandao wake a Instagram ambao unasomeka, “Wha’s the one thing you would love to teach the world.”
Hata hivyo Adebayor alishindwa kuvumilia na kuamua kucomment kwenye ujumbe huo kwa kuandika, “Make all those things start from you” na pia aliweka comment nyingine inayosema, “How to respect people opinion.”
Lakini baya zaidi lililoonyesha penzi la wawili hao kutawaliwa na ua jeusi baada ya kila mmoja kum-unfollow mwenzake.
Comments