Hussein Ndubikile,Pwani
Baraza la Ardhi na Nyumba la Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa
Pwani limesema Julai 26 mwaka huu litaanza kuisikiliza kesi ya msingi ya
mgogoro wa ardhi kati ya Mwanasheria
Mkuu wa Serikali(AG), Adelardus Kilangi ambaye ni mdai dhidi ya wadaiwa zaidi ya
70 ambao ni wananchi wa Kijiji cha Vicheji kilichopo wilayani humo.
Hatua hiyo imdikiwa jana wakati Mwenyekiti wa baraza hilo Mwakibuja
alipokuwa akisoma uamuzi wa mapingamizi yaliyowasilishwa na pande mbili katika
shauri hilo.
Akisoma uamuzi huo leo wialyani humo, Mwenyekiti Mwakibuja aliitupilia mbali
hoja ya mdai Kilangi ambayo iliwasilishwa kwa maandishi barazani hapo kupitia
wakili wake Daudi Maginge Kuwa wadaiwa hawana nguvu ya kumshtaki..
" Baraza linatupilia mbali hoja hiyo kwa kuwa kila raia ana haki ya
kushtaki na kushtakiwa,' Anadai Mwenyekiti Mwakibuja.
Pande mbili zilwasilisha mapingamizi mbalimbali kwa maandishi huku wadaiwa
wakiliomba baraza limuongeze mwenyekiti wao wa kijiji Ramadhani Maulid katika
shauri hilo ombi ambalo lilitupiliwa mbali kwa kukosekana vielelezo vya
kutosha.
Mgogoro katika kesi namba 55 ya mwaka 2016 unawahusisha wadaiwa Said Kaisi 46, Bakari Saguti 60, Omary Issa 42, Juma Omary 40, Salima Bilali (53), Regia Issaya(55) ,Sada Abdallah(72) na ambao kwa pamoja wanadaiwa kuingia kwenye shamba la Kilangi bila kibali.
Washitakiwa hao kwa pamoja inadaiwa kuwa Mei 9 2016 katika Kijiji cha Vicheji waliharibu Miti 13 ya Minazi na nyumba mbili vyenye thamani ya Sh. Mil 22.2 mali ya AG Kilangi.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi julai 26 mwaka huu itakapokuja kwa ajili ya kuanza kusikilizwa ambapo nje ya mahakama wadaiwa waliulalamikia uongozi wa baraza hilo kwa kuwachanganya haswa pale muda wa kesi kuanza tofauti ilivyopangwa awali.
Akizungumzia suala la muda kwenda tofauti mdaiwa Saidi Kaisi amesema baraza limekuwa likipangua muda wa kesi yao bila taarifa hali inayowanyong'onyeza na kuwafanya wajiulize maswali mengi kuhusiana na mwenendo mzima wa kesi.
" Tunafahamu kuw kesi yetu tunapambana na mtu mkubwa serikalini lakini kwakuwa serikali yetu ni sikivu tunaimani mahakama itatenda haki,'amesema kaisi
Naye Jonas Kyando ambaye ni mdaiwa amebainisha awali waliambiwa kesi hiyo ingsikilizwa muda wa saa 5 asubuhi lakini cha kushangaza saa 4 asubuhi uamuzi ulitoka bila kuambiwa hali inayowaweka njia panda kupata haki yao.
Hata hivyo wanakijiji wengine waliungana kma pamoja kuomba haki ya wanyonge isidhulumiwe.
Comments