IDARA ya Huduma za Kinga ya Wizara ya Afya ,Maendeleo
ya Jamii ,Jinsia ,Wazee na Watoto imesema ugonjwa wa Ebola ni janga
hivyo serikali imejipanga kukabiliana nao.
Ugonjwa huo ambao tayari umeripotiwa kuwapo Jamhuri ya
Kidemokirasia ya Congo (DRC) tangu mei 8 mwaka huu na hadi kufikia sasa
watu 51 wameri potiwa kupata maambukizi na 27 kati yao wamefariki dunia.
Hayo yamesemwa Jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki
iliyopita na Kaimu Mkurugenzi wa Idara hiyo Dkt.Khalid Massa wakati wa
kikao cha tathimini kati ya Kamati ya Kitaifa ya kukabiliana na
magonjwa ya Mlipuko.
Alisema Tanzania tumewekwa nafasi ya pili miongoni mwa nchi
zenye uwezekano wa kupata maambukizi ya ugonjwa huo kwa haraka kwa
kuwa tupo jirani na DRC .
"Ugonjwa huo ulishawahi kutokea miaka ya nyuma katika
baadhi ya nchi zilizopo Barani Afrika na katika kipindi hicho waliweza
kuwapa mafunzo wataalamu wao na wapo walio kwenda kusaidia katika baadhi
ya nchi ,"alisema Dkt. Massa.
Alisema tathimini ya Shirika la Afya Duniani imeonesha
tupo katika rangi ya kijani ikimaanisha vizuri kuukabili ugonjwa huu na
kuwa wamejiandaa vizuri kuukabili ugonjwa huo na tayari wanayo miongozo
mbali mbali waliyo andaa na wameandaa mipango madhubuti sambamba na
kuwa wamejitaidi kuweka gharama ya kuukabili ugonjwa huo usifike
nchini.
Tiba ya Ebola
Aidha Dkt.Massa alisema Wizara imepokea mapendekezo
yaliyotolewa na maofisa wa WHO ikiwemo hiyo ya mafunzo zaidi na elimu
kwa umma jinsi ya kuepuka kupata maambukizi ya ugonjwa huo ikiwa na hali
ya kuzitam bua dalili sake.
Aliongeza kuwa bado nchini Congo watu 28 hadi sasa wanaripotiwa kuwa
kuwa nao wameambukizwa katika idadi ya kuenea kwa ugonjwa huo iliyofikia watu 51.
kuwa nao wameambukizwa katika idadi ya kuenea kwa ugonjwa huo iliyofikia watu 51.
Wakati huo huo akizungumza kwa niaba ya mwakilishi wa WHO
Kanda ya Afrika (AFRO) na mwakilishi wa WHO Uganda Dkt.Miriam Nanyunja
alisema wamefanya tathimini tangu Mei 21 hadi 25 mwaka huu.
Alisema Tanzania imewekwa nafasi ya pili pamoja na mataifa
mengine ikiwemo Angola,Rwanda,Burundi pamoja na Sudani Kusini na
Zambia.
"Sasa jamii ipewe elimu kutosha na ikiwa wataalamu watapewa
mafunzo na kujiweka katika nafasi nzuri zaidi kuzuia kuzuia usiingie
zaidi nchini hapa,"alisema.
Ugonjwa wa Ebola ni janga linapo kuwa katika nchi yoyote
linatajwa kuwa janga la dunia na ndio maana hatua za mapema
zinachukuliwa kwa uzito mpana ndio maana WHO wapo nchi hapa kuangalia
mipango ya kuukabili usiingie.
Comments