Katibu Mkuu wa Klabu ya Yanga, Charles Boniface Mkwasa ametoa
ufafanuzi juu ya wachezaji wake muhimu, Kelvin Yondani, Obrey Chirwa,
Ibrahim Ajib na Papy Kabamba Tshimbi kutojumuika na kikosi kilichosafiri
juzi kuelekea nchini Algeria kwaajili ya mchezo wao wa hatua ya makundi
dhidi ya USM Alger.
Mkwasa amesema kuwa wachezaji wote waliyoshindwa kujiunga na Yanga
kwenye safari hiyo walikuwa na sababu zao muhimu nawala siyo mambo
mengine kama yanavyoelezwa.
Kunasababu mbalimbali kwa wachezaji kupelekea wao kutokusafari, rabda nikianza na Kelvin Yondani yeye alipata majeraha wakati wa mechi na Simba na alipoomba atoke tukashindwa mkutoa kwasababu mechi ilikuwa tayari ilishamalizika.Mchezaji wa pili ni Obrey Chirwa alikuwa na Maleria na baada ya mechi ikaongezeka kwahiyo ikashindikana kusafiri.Mchezaji wa tatu ni Ajib, yeye yupo fiti ila anamatatizo ya kifamilia Mkewake anatarajia kujifungua muda wowote na hivyo kunahitaji uwangalizi wa hali ya juu kwahiyo anahitajika awe karibu ndiyo maana hakuweza kusafiri.Papy Kabamba Tshimbi alikuwa pia amepata majeraha kutoka Ethiopia na hata mechi na Simba alikuwa amecheza na akaomba atoke kwakuwa majeraha yalikuwa yameongezeka kwahiyo hakuna kitukingine chochote kimetokea kama watu wanavyodai mtaani kwakuonyesha kuwa kuna kitu chochote huo ndiyo ukweli uliyokuwepo kwahiyo niaombe wanachama wawe na utulivu katika kipindi hiki na tuwe na umoja ili tuhakikishe tunapata matokeo mazuri ugenini kwakuwa ni mechi ya kwanza isituvunje nguvu na watambue kuwa vijana waliyokwenda wanaaminika na wana uweledi mzuri.
Yanga itashuka dimbani siku ya Jumapili kuanza kutupa karata yao ya
kwanza kwenyemchezo huo wa kwanza wa hatua ya makundi wakiwa ugenini
dhidi ya USM Alger ya nchini Algeria.
Comments