SERIKALI imeiweka benki ya kibishara ya Twiga Bancop chini
ya uangalizi wa benki ya posta ambayo inamilikiwa na benki
kuu nakutaka benki hiyo kuungana
na benki ya posta nakuwa benki moja .
Hatua ya serikali kuweka benki ya Twiga Bancop chini yauangalizi
wa benki kuu imetokana na benki hiyo kuwa na upungufu mkubwa wa
mtaji kinyume ya matakwa ya sheria ya mabenki na taasisi za fedha
ya mwaka2006 hali iliyotokana na benki hiyo kuwa usalama mdogo wa
sekta ya kifedha katika benki hiyo .
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Naibu Gavana
wa benki kuu Benard Gese amesema kuwa katika kuhakikisha sekta yakibenki
inaimarika serikali imeamua kuimarisha usimamizi wake dhidi ya benki hiyo
kwa kuunganisha na benki yaposta ambayo pia inamilikiwa na serikali .
''Kwamujibu wakifungu cha 30 (1)a cha sheria yamabenki na taAsisi
zake ya mwaka2006 benki kuu ya tanzania imeidhinisha benki yatwiga na tpb
kuwa benkimoja kuanzia leo ''Alisema Naibu Gavana Gese .
Imeelezwa kuwa BOT ilichukua usimamizi wa benki ya Twiga baada ya kubaini
upungufu mkubwa wa mtaji kinyume na matak wa ya sheria ya mabenki,
Shughuli zote za kibenki za banki hiyo zilisimamiwa na msimamizi
kutoka Benki Kuu ya Tanzania.
kwa upande wake Rosemary Mtenga ambaye ni meneja uendeshaji Bodi
ya Bima alisema kwa sasa wapo katika mchakato wa kufanya ukaguzi
wa madeni ili kuhakikisha wadaiwakiwemo wanahisa za makampuni.
Alisema zoezi hilo la kufanya ukaguzi wa madeni na kuwalipa
wadai linaendana na kuwalipa bima.
"Zoezi hili limefanikiwa kwa asilimia 60 ambapo shilingi milioni 1.5
wataziweka katika ofisi za matawi yao ya benki ili waeweze kulipwa
mwisho wa mwezi huu,"alisema Mtenga.
Alisema vizuri benk kuungana ili kuhakikisha riba zinapungua
benk kama CRDB tayarizimeanza kufuata mwelekeo huo ambapo benki
kuu inahakikisha mazingira ya ushindani wa kibiashara yanakuwa
wezeshi kwa kila benk zakibiashara ili kudhibiti ongezeko
la riba kwenye mabenki.
"Katika kipindi cha mwezi Januari mwaka huu benki kuu ili zifuta
leseni za benki tatu taratibu zinaendelea kwa mfirisi na hadi kufikia
Juni 30 mwaka jana benki tano ziliweza kufutiwa leseni ," alisema Mtenga.
Comments