KAMPUNI ya Mabasi inayotoa huduma katika mabasi yaendayo haraka Dar esSalaam UDA -UDART unatarajia kuhamishwa kalakana yao iliyopo Jangwani Wilayani Ilala.
Hayo yalisemwa Dar es Salaam leo na Mkuu wa Kitengo cha mawasiliano UDART Deus Buganywa wakati wa kuzungumza na waandishi wa habari kuelezea athari za mvua za mafuriko zilizopekekea kuharibu mfumo wa miundombinu ya umeme.
"Udart tunatarajia kuhamisha mradi wetu eneo la Jangwani kutokana na athari kubwa zinazoendelea kupelekea mradi kupata hasara"alisema Deus.
Deua alisema kwa sasa Menejiment ya Uongozi wa UDART wapo katika mchakato wa kutafuta eneo lingine la kuweka kalakana hiyo kutokana na eneo la Jangwani mifumo yote ya umeme imeharibika kupelekea kuhamisha mabasi ambapo kwa sasa yupo Gerezani na Kimara.
Alisema mvua ya kwanza kubwa ilianza Aprili 14 na mvua nyingine Mei 4 zimeleta athari eneo la Jangwani na bado mvua zinazoendelea .
Alisema mafuriko hayo ya juzi ni makubwa tofauti na mengine yamepelekea tope kujaa eneo hilo UDART ina mabasi 140 mabasi 29 yamekwama jangwani yanaitaji matengenezo mabasi 129 yapo Gerezani na Kimara kwa sasa.
"Ajali hiyo ya Mafuriko kwa sasa mifumo ya Umeme imekufa visima vya mafuta vilivyopo Jangawani haifanyi kazi Udart inarazimika mabasi yao kujaza katika vituo vya mafuta vya nje "alisema.
Mradi wa awamu ya kwanza wa Udart unaitaji mabasi 375 gari 70 kwasasa zipo bandarini zitaingia barabarani mda wowote .
Comments