Bodi ya mikopo ya elimu ya juu imesema mpaka kufika robo tatu ya mwaka wa 2017/18 Wamefanikiwa kukusanya kiasi cha shilingi bilioni 132.
Akizungumza na wandishi wa habari jijini Dar es salaam Kaimu mkurugenzi msaidizi wa urejeshaji mikopo Phidelis Joseph amesema kuwa kwa mwaka 2006 walikuwa wakikusanya kiasi cha shilingi bilioni 2 kwa mwezi lakini mpka kufika sasa wamekuwa wakikusanya shilingi bilioni 15 kwa mwezi na kudai kuwa bado wanadai kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni 250 ambazo bado ziko nje.
Aidha amewaomba waajili kuhakikisha wanawakata kiasi cha asilimia 15% cha mshahara wa wajiliwa wao.
Bodi ya mikopo ya elimu ya juu Imekuwa na kampeni ambayo iliweza kuwafikia zaidi ya waajiliwa 80 na taasisi mbalimbali na kuhamsisha namna ya utaratibu wa urejeshaji mikopo na kampeni ilianza jijini Dar es salaam ikafata Dododoma,mwanza na kwasasa inaelekea Zanzibar
Comments