MSANII wa filamu nchini Marry Nicolous a.k.a Baby ambaye amekamilisha ujio wa filamu kama Nguvu ya Neno,Chimvula,Haiba ya Moyo amesema kuwa katika muda mchache kuanzia sasa zitaanza kuoneshwa kupitia Dstv.Moja ya ushawishi mkubwa kuona kazi ya msanii inakuwa katika kiwango bora ni kazi ya msanii kukubalika kuoneshwa katika channel kubwa .
Akizungumza na mwandishi wa gazeti hili Dar es Salaam Baby amesema katika nyakati za sasa wasanii wamekuwa wakifanya biashara na vituo vya luninga kubwa kama channel ya Dstv ila wanachukua filamu zenye ubora mkubwa.
Alisema anafurahishwa na hali ya kupokelewa vyema kwa filamu zake katika luninga hiyo iliyopo Afrika Kusini kwa mkataba na channel hiyo utakuwa wenye maslahi mazuri.
"Mania ya kufikia malengo mengine makubwa sana katika anga za filamu , mara tu filamu hizo zitakapoanza kurushwa katika luninga hiyo kubwa barani Afrika kazi zangu nyingine zitafuata nimepania kuwa mwanamke mwenye muonekano mzuri wa kimafanikio kupitia sanaa ya filamu,"alisema Baby.
Baby alisema kupitia kampuni yake iitwayo Marry Nicol Film Campany ameanza kuandaa pia ujio mwingine uitwao 'Mtukufu Ramadhani' chini ya director Kebby Kazingini.
Filamu zingine zijazo amezitaja kuwa ni Moyo Mkakamavu pamoja na nyingine iitwayo Mzazi wa Tatu ambapo amefafanua kuwa mpaka kufikia mafanikio ya kuandaa filamu zake ameisha shirikishwa kwenye filamu zingine awali hatua iliyomjenga kiuwezo latika anga hizo.
Comments