Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Ashantu Kijaji amezindua Programu tatu za huduma za Bima na hifadhi za jamii katika Chuo cha IFM
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Ashantu Kijaji amezindua
Programu tatu za huduma za Bima na hifadhi za jamii katika
kitivo cha bima na hifadhi za jamii cha Chuo cha Usimamizi
wa Fedha (IFM).
Shahada ZA uzamili zilizinduliwa ni Master of Scence in Social
Protection Policy and Development , Master of Science Isuarance
and Acturial Science pamoja na bachelor of Science in Acturial
Sciences.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Dar es Salaam hivi karibuni
Dr Kijaji alisema kuzinduliwa kwa programu hizi ni mkombozi
kwa watoa huduma ya bima kwani sekta bima na hifadhi ya jamii ni ndogo
kutokana na wananchi kukosa elimu na kufanya sekta ya bima na hifadhi ya
jamii kuchangia asilimia moja katika pato la Taifa.
"Mchango wa sekta ya bima katika uchumi ni mdogo kutokana na uelewa
mdogo wa wananchi jambo ambalo litapunguzwa na kupata wasomi wengi
wenye weledi mkubwa katika huifadhi wa jamii,"alisema.
Alisema wataalam hawa watakao zalishwa nidhahili wataongeza wateja
watumia huduma za bima katika nyanjazote kwani tayari wanao ushawishi
mkubwa na mbinu za jinsi ya kuelimisha wananchi, wakaelewa umuhimu
wa kutumia bima.
Kwa upande wake mratibu wa programu hizo Zubeda Chande ambaye pia ni
Mkufunzi katika Idara ya Hifadhi ya Jamii pamoja na bima amesema
kwa kiasi kikubwa programu hizo zitakuwa na mchango mkubwa wa kuelimi
sha Umma umuhimu wa kununua bima na kujiunga na mifuko ya hifadhi ya
jamii ambayo awali watu wanaonekana kutoipa kipaumbele katika maisha
yao ya kila siku.
"Sisi kama menejimenti ya IFM tumefanya utafiti na kugundua watu wengi
hapa nchini hawajajiunga na huduma za bima pamoja na hifadhi za jamii,
utafiti huu tumefanya katika nyanja zote za bima hali ambayo imetoa
msukumo kuanzisha programu hizi ambazo kwazo huduma za bima na hifadhi za
za jamii zitasambaa kwa kiasi kikubwa kwa wananchi kwani wanafunzi
wetu tunawawezesha kifedha kuwazungukia wananchi mikoani na kufanya
utafiti juu ni kwanini watu wengi hawataki kununua bima au kujiunga
na mifuko ya hifadhi ya jamii,"alimaliza Chande.
Pichani ni Mohammed Jaffer ambaye ni rais wa chama cha madalali wa
Bima
Naye mwanafunzi wa kituvo hicho Donald Masai alisema kufikia mwaka
2025 uchumi wa Tanzania utakuwa umefikia uchumi wa kati ambao utawezesha
kila mwananchi kuchangia pato la Taifa kupitia matumizi ya bima.
"Katika suala zima la ukuaji wa uchumi lazimaukutane na changamoto nyingi
ambazo kimsingi ukitaka usiumize akili katika masuala muhimu ya maisha
wewe jiunge na bima ambazo zitakupunguzia maumivu katika yote unayofanya
na unayokusudia kwani yakikwama kwa changamoto zilizokinyume na uwezo
wako bima inakulipa unaanza upya,"alisema Masai.
Wanafunzi watakao fuzu vyema programu hizo watafadhiliwa na Umoja
wa Ulaya kwenda kusoma nje kwa kupata weledi zaidi.
kwa upande wake Mohammed Jaffer ambaye ni rais wa chama cha madalali wa
bima alisema kwa nchi zinazoendelea kiuchumi kama Tanzania,ilikufikia
uchumi wa viwanda ni vyema kila mwananchi kutumia huduma za Bima
katika nyanja zote hili apate kuishi kwa amani.
Comments