Mstahiki Meya wa jiji la Dar es salaam Iaya Mwita (kushoto),Mkurugenzi wa Jiji la Dar es salaam (kulia)wakiongoza baraza la madiwani
Halmashauri ya jiji la Dar es salaam imeweka mikakati ya mpango wa kutekeleza miradi miwili ya kimaendeleo ikiwemo uboreshaji miundombinu ya jiji pamoja na usafirishaji.
Hayo yameelezwa leo na Mstahiki Meya wa jiji la Dar es salaam na Mwenyekiti wa baraza la madiwani Isaya Mwita wakati alipokuwa akizungumza katika kikao cha baraza la madiwani kilichojadili taarifa ya robo ya tatu ya mwaka.
Mstahiki Meya Mwita amesema mpango wa miundombinu ya jiji la Dar es salaam ilipangwa tangu mwaka 1977 hivyo kwa wakati huu watawajengea uwezo viongozi kuweza kufahamu uwezo wa namna ya kupanga mpango kazi wa jiji.
Mbali na mipango hiyo mjumbe wa baraza hilo,Abdallah Mtinika amehojii kuhusu mgogoro uliopo baina ya Jengo la biashara la Machinga Complex dhidi ya Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) ambapo Mstahiki Meya amejibu na kutolea ufafanuzi kuwa deni wanalodaiwa kutoka kwenye mfuko huo umefikia Sh57bilioni.
Comments