ASKOFU wa dayosisi ya mashariki na pwani Dr.Alex Malasusa jana amezindua jengo
la kanisa la ushirika wa kimara lenye thamani ya shilingi billion 5.1 na kuhimiza
ushirikiano,upendo na amani katika kuleta maendeleo.
Mbali na hilo Askofu amezindua shule ya awali na msingi ya Jerusaremu sambamba
na kuweka jiwe la msingi katika kituo cha kulelea watoto yatima na hospitali
itakayotoa huduma mbali mbali ikiwemo rufaa .
Tukio hilo lilitokea jana Dar es Salaam na kuandika historia kubwa ya kipekee katika
ujenzi wa makanisa hapa nchini ambapo wageni kutoka makanisa mengine walihudhuria
sambamba na kutoa salamu zao .
Askofu alisema makanisa yapo duniani kwaajili ya kusambaza upendo kwa watu wote
na uponywaji wa kiroho ambapo mwanadamu haponi kwa sindano na vidonge bali uponywa
kwa neno la Mungu.
"Kanisa lazima kitovu cha upatanishi hivyo wakazi wa eneo hili dumisheni upendo
katika kumtumikia Mungu na kuwa chachu ya maendeleo na kuwa wazazi wapeleke
watoto wao katika nyumba za Ibada hili wapate kumtumikia Mungu wakingali wadogo
na kukua katika maadili mema ya kumcha mwenyezi Mungu,"alisema Askofu Dr.Malasusa .
Dr.Malasusa alisema kanisa hilo liwe kiu ya uhadilifu na kumpongeza mchungaji
kiongozi wa Ushirika wa Kimara Mchungaji Willbroad Mastai kwa ukamilishi wa
ujenzi wa kanisa hilo ambapo aliwataka makanisa mengine kuiga mfano huo.
Katika taarifa za uwasilishwaji kutoka katika kanisa hilo zilizotolewa na Ushirika
wa Kimara zilisema kuwa awali kanisa hilo lilikuwa limejengwa kwa miti na kukandikwa kwa
udongo ambapo idadi ya washiriki ilikuwa ikiongezeka nandipo Kanisa la matofali lilipo
jengwa.
Hakitoa taarifa ya mipango mikakati ya Ushirika wa Kimara Dkt.Evelyn Mduma alisema
mipango mikakati hiyo ililenga kukamilisha mkakati wa Jimbo na hatimaye Dayosisi ya
Mashariki na Pwani.
Alisema kanisa hilo limekuwa likikamilisha kwa kutoa huduma mbali mbali za kijamii ikiwemo
kuwalipia ada na kutoa matumizi mbali mbali ya wanafunzi, kununua sare za shule na vitabu
kwa watoto yatima,pia kutoa misaada kwa wanaopata majanga mbali mbali na kutoa sadaka kwaajili
ya wagonjwa wa Kansa pamoja na kutoa misaada ya kibinadamu kwa wajane.
Comments