Msanii nyota kwenye muziki wa Hip Hop nchini Fid Q ametumia siku ya Wafanyakazi kutoa ombi hilo kwa Wizara ya Habari, Utapduni, Sanaa na Michezo, ikiwa ni siku moja tu tangu ateuliwe na Chama cha Muziki wa Kizazi Kipya Tanzania (TUMA), kuwa Mwenyekiti wa kamati ya Fedha, Mipango na Uchumi.
“Sanaa ni sekta rasmi hivi sasa lakini bado haijapewa sera na hiyo ni sawa na kuwa na ofisi isiyokua na KANUNI, TARATIBU wala SHERIA. Kwa ufupi bado tunaongozwa na sera ya utamaduni. Tunayofuraha kubwa ya kuitumia sikukuu hii ya wafanyakazi kwa kuikumbusha WIZARA na SERIKALI kwa ujumla kutuundia sera ili SANAA yetu iweze kuleta tija kwenye jamii. (Na katika hilo tunashauri RASIMU iandaliwe na WASANII wenyewe). ameandika
Comments