JOSE MOURINHO
anadaiwa kuidhinisha makubaliano ya usajili wa pauni milioni 80 wa
kiungo wa Lazio Sergej Milinkovic-Savic kwenda Manchester United.
Kocha huyo wa United amefanikisha mazungumzo yaliyofanyika wiki
iliyopita ambayo yamenyoosha njia ya Sergej Milinkovic-Savic kuelekea
Old Traffiord.
Sergej, 23, raia wa Serbia, anakwenda Old Trafford kuimarisha safu ya
kiungo ambayo itakuwa bila Michael Carrick anayestaafu na Marouane
Fellaini ambaye amekataa mkataba mpya wa kuendelea kutimukia kuitumikia
Manchester United.
Comments