Kamanda
wa Polisi mkoa wa Pwani Jonathan Shanna ameelezea jinsi walivyomtua
mzigo mwizi aliyeganda na kiroba cha mahindi alichoiba huko Mlandizi
Kibaha.
Mapema leo kijana huyo aitwae, Frank Joseph mwenye umri wa miaka 23
mkazi wa Mbezi alijisalimisha polisi baada ya kuiba mzigo wa mahindi na
kushindwa kuutua.
Kamanda Polisi amesema baada ya kijana huyo kumuona walifanya naye
mahojiano na kukiri kuiba mzigo huo na kila walivyojaribu kuuondoa mzigo
huo kijana huyo alipiga kelele za maumivu hali ambayo iliwafanya
wamuache na kumtafuta mtu aliyeibiwa.
“Mnamo tarehe 3 mwezi wa tano mwaka 2018 majira ya saa 12 na dakika
45, huko katika kata ya Mlandizi Wilaya ya Kibaha na mkoa wa Pwani
tulipata taarifa toka kwa mwenyekiti wa Mlandizi ndugu Ally kwamba kuna
mtu asiyefahamika amekutwa amebeba mahindi yanayokadiriwa kuwa na uzito
wa kilo 20 na ameshindwa kuyatua toka kichwani na wakati huo huo
akaendelea kutueleza kwamba amezungukwa na watu wenye hasira wanataka
kumuadhibu. Baada ya kupata taarifa hiyo tulifika eneo la tukio na
kukuta kweli mtu huyo yupo na amebeba mahindi, tulimuamuru azitue chini
lakini akashindwa na pia tukajaribu kumtua lakini tukashindwa kutokana
na kelele za maumivu alizokuwa akizitoa,” alisema Kamanda.
Baada ya zoezi hilo kushindikana jeshi la polisi lilimwita mtua
ambaye anadaiwa kuibiwa na kufanya manjonjo yake na muda mchache akamtua
kijana huyo zigo la mahindi.
Polisi wamesema kwa sasa wapo kwenye jitihada za kumpandisha
kizimbani kijana ambapo pia wamewataka wananchi kuepuka matukio ya
kihalifu.
Comments