Halmashauri ya Manispaa ya Ilala imeagizwa ndani ya siku 45 kulifanyia ukarabati wa miundombinu katika Soko la Kimataifa la Samaki la FErry.
Wziri wa nchi ofisi ya Rais serikali za mitaa Tamisemi Mhe. Suleiman Jafo,akizungumza na viongozi pamoja na wafanyabiashara wa Soko la Samaki la Feri
Agizo hilo limetolewa leo jijini Dar Salaam na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala
za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo katika ziara aliyoifanya sokoni hapo ambapo alikagua miundo mbinu mbalimbali ikiwemo barabara ya soko ,meza, choo pamoja na maji
Amesema kwa kuwa wafanyabiashara soko hilo wanalipa kodi hivyo ni
wana haki ya kupatiwa miundo mbinu rafiki na salama.
Akitoa maagizo hayo amesema ndani ya siku hizo mazingira yanatakiwa
yarekebishwe na kumtaka Injinia ahakikishe barabara hiyo imetengenezwa
hadi kufikia Julai 23 atakaporudi kuangalia utekelezaji ukarabati wa miundo mbinu hiyo.
Amesema soko hilo kubwa ambalo linakuza uchumi wao na wa nchi kwa
ujumla anataka wakina Mamantilie waliokuwa wakifanya biashara katika eneo
hilo na kutolewa warudishwe na kuwataka akina Mamantilie hao kufuata
sheria na kuwa mlinzi kwa kila mmoja kuhakikisha wanaofanya biashara
za madawa ya kulevya wanabainishwa.
"Waliokuwa wanafanyabiashara ya chakula hapa Sokoni warudishwe na
kuendelea na kazi zao ili kuwarahisishia wafanyabiashara kupata
chakula kwa wepesi."amesema Jafo.
Aidha amemtaka Meneja soko hilo, B. Hanje wa kuhakikisha wanatenga sehemu za
wakina Mama Ntilie ili waendelee kufanya biashara kutokana na kutolewa maeneo
hayo kwa tuhuma za kujihusisha
na madawa ya Kulevya.
Amemtaka pia Meneja wa Soko hilo kuhakikisha anatenga sehemu maalumu
ya kina Mamantilie ili waweze kuendeleza biashara yao na wanaofanya
shughuli zao hapa waweze kuwa na uhakika wa
kupata chakula sehemu salaam .
kWA upande wake Mwenyekiti wa bodi ya soko hilo ,Henry Masaba
amesema kuwa mara baada ya agizo hilo la kuboresha miundombinu wao
kama viongoziwa soko hilo watahakikisha wanafanya jitihada ili
kuboresha miundo mbinu hiyo.
Ameongeza kuwa watashugulikia changamoto zilizopo katika soko
hilo ili kustawisha biashara zao na kujipatia
kipato cha kuendesha maisha yao.
Meneja wa Soko hilo amefafanua kuwa kuna Jengo ambalo lipo katika soko
hilo na kwamba linadaiwa kuwa ni la halmashauri ya Manispaa ya
Ilala ambapo hawakusanyi Kodi kutoka katika jengo hilo hivyo wanashindwa
kulikarabati kutokana na kuwa liko chini ya manispaa.
wafanyabiashara wa soko hilo wamekiri kuwepo kwa changamoto
mbali mbali ,na na kushukuru ujio huo wa Waziri , kwa kufika
na kuwasaidia ili changamoto zao ziweze
kutatuliwa .
Comments