Baada
ya mchezo wake wa kirafiki dhidi ya Dodoma Combine kumalizika Uwanja wa
Jamhuri kwa sare mabao 2-2, mabingwa wapya wa Ligi Kuu Bara kwa msimu
wa 2017/18 Simba SC, jana walifanyiwa hafla ya mlo wa jioni na wabunge
wanaoishabikia timu hiyo.
Kikosi hicho kilifanyiwa hafla fupi na
wabunge ambao wanaishabikia Simba kwa kujumuika nao katika chakula cha
jioni jijini Dodoma.
Simba ipo Dodoma baada ya kuwasili jana
ikitokea mjini Singida kushiriki mchezo wa ligi ambapo ilifanikiwa
kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Singida United.
Baada ya kuwasili jijini humo jana na
kujumuika katika mlo wa jioni na wabunge, kikosi hicho kimepata mwaliko
wa kwenda bungeni leo kupata pongezi baada ya kufanikiwa kuwa mabingwa
wa ligi.
Simba watapata wasaa wa kuhudhuria
kikao cha leo katika Bunge la Jamhuri ili kupata pongezi zao baada ya
kuchukua ubingwa huo wakiwa hawajapoteza mchezo hata mmoja.
Simba watakuwa wanaweka rekodi ya kufika Bungeni ikiwa ni mara ya kwanza tangu Dodoma ipewe hadhi ya kuwa jiji.
Comments