Watumishi wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi wameaswa kuijiepusha na vitendo vya rushwa ili kuendelea kuongeza tija.
“Hatuwezi kutoa haki kama tunapokea rushwa hivyo naagiza kila mtumishi awe mlinzi wa mwenzake, ukimwona mtumishi mwenzako anajihusisha na vitendo hivyo ni vyema akachukua hatua ya kutoa taarifa kwa mkuu wako wa kazi ili hatua stahiki zichukuliwe,” alisisitiza Mabula.
Aidha Mabula alisema kuwa ni vyema watumishi wote wakajitathmini ili kuona ni wapi tunahitaji kujipanga upya ili kukidhi matarajio ya watanzania katika huduma zinazotolewa kwa wananchi.
Hata hivyo, Mabula alitoa wito kwa watumishi wote kuendelea kufanya kazi kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na taratibu za Usimamizi wa sekta ya Ardhi nchini.
Comments