Diwani wa Kata ya
Kijichi Eliyasa Kasim Mtarawanje
Jumla ya vijana wapatao
200 wa kata ya Kijichi iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Temeke jijini Dar es
salaam wamepata fursa ya kusoma mafunzo ya kompyuta ili kuendelea kukuza wigo wa
kujiendeleza kiuchumi.
Mafunzo hayo ambayo yanatolewa bure katika kata hiyo ikiwa ni Moja ya
mikakati ya kimaendeleo inayofanywa na Diwani wa Kata ya Kijichi Eliyasa Kasim
Mtarawanje katika kuhakikisha vijana wanajipatia ujuzi utakaowasaidia kuweza
kujikwamu kiuchumi katika ufanyaji wa kazi.
Akizungumza jana Dar es Salaam Diwani Mtarawanje alisema amewatafuta
wafadhili Digital Oportunity Trust (DOT) ili kuweza kuwasaidia vijana kuweza
kujifunza mafunzo ya elimu ya kompyuta.
"Tunawashukuru sana hawa watu wa DOT kwa kutupatia fursa hii kwani
takribani ya vijana 60 tayari wameshahitimu na wamepewa vyeti vyao,ambapo kila
mtaa wametoka vijana 12 na ndani ya vijana hao 12 tumewapeleka vijana kufanya
kazi na huku wengine kati yao nimewafungulia steshenari ili waweze kuiendesha na
tutaiita Kijichi Stationer yuoth Center"amesema Diwani
Mtarawanje
Aidha amesema wamepata wafadhili waitwao Open Mind ambao mpaka sasa
wamekwisha wafundisha wakina mama 70 elimu ya ujasiriamali nao waweze kuboresha
bidhaa zao na kujikwamua kiuchumi.
Kwa upande wake Mjumbe wa serikali ya mtaa mtoni kijichi Hanifa Idd
Rashid anasema mafunzo hayo yamewajengea vijana wa kata hiyo pamoja na kina mama
wajasiriamali kupata hamasa ya kujifunza mambo mbalimbali ili yaweze kuwasaidia
kwenye maisha yao.
Baadhi ya vijana ambao
wamepata fursa ya kupata mafunzo ya elimu ya kopyuta Peter Martin pamoja na na
Hamis Abubakari wanasema ni vyema vijana wakajiwekea mazoea ya kujifunza elimu
hiyi iki kuweza kufahamu yanayoendelea katika dunia hii.
Hata Hivyo Diwani
Mtarawanje amewataka wananchi wa kata ya Kijichi kuendelea kuonyesha umoja na
ushirikiano kwa viongozi wao ili waendelee kufanikisha mikakati waliyoipanga kwa
wakati ya kuifanya Kata hiyo kuwa ya kisasa na ya mfano katika Manispaa ya
Temeke.
Comments