Mshambuliaji wa kimataifa KRC Genk Mbwana Samatta ameifungia mabao mawili ikiibuka na ushindi wa 4-1 dhidi ya Sporting Charleroi.
MWAMBA WA HABARI
NA MWANDISHI WETU.
MSHAMBULIAJI
wa kimataifa Tanzania, Mbwana Ally Samatta usiku wa Jumapili amecheza
muda wote na kuifungia KRC Genk mabao mawili ikiibuka na ushindi wa 4-1
dhidi ya Sporting Charleroi katika mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza A
Ubelgiji Uwanja wa Luminus Arena mjini Genk.
Samatta
amefufua makali, baada ya kucheza bila kufunga kwa muda mrefu
‘alifungulia mbwa’ Alhamisi alipotokea benchi na kufungia bao la
kusawazisha KRC Genk ikipata sare ya 1-1 na AA Gent katika mchezo wa
Ligi pia Uwanja wa Luminus Arena.
Na
leo Samatta ameendeleza moto wake kwa mabao yake aliyofunga dakika za 24
na 61, wakati mabao mengine ya Genk yamefungwa na Leandro Trossard
dakika ya 34 na Dieumerci N'Dongala dakika ya 77, wakati la kufutia
machozi la Sporting Charleroi limefungwa na Cristian Benavente dakika
ya 31.
Alhamisi
Samatta aliingia uwanjani dakika ya 54 kwenda kuchukua nafasi ya
mshambuliaji Mgiriki, Nikolaos Karelis wakati huo tayari Gent wanaongoza
kwa 1-0, bao lililofungwa na mshambuliaji kutoka Japan, Yuya Kubo
dakika ya 15 akimalizia kazi nzuri ya kiungo kutoka Georgia, Giorgi
Chakvetadze.
Samatta
akafunga bao lake dakika ya 66, ambalo lilikuwa la kwanza tangu Oktoba
25, mwaka jana alipofunga bao la pili katika ushindi wa 2-0 dhidi ya
Club Brugge katika Ligi Daraja la Kwanza A Ubelgiji, Uwanja wa Luminus
Arena pia.
Lakini
leo Samatta ameanza na kumaliza mechi akifikisha mabao 25 katika mechi
yake ya 88 tangu Nahodha huyo wa Taifa Stars ajiunge na Genk Januari
mwaka 2016 akitokea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
(DRC).
Kikosi
cha KRC Genk kilikuwa; Vukovic, Nastic, Colley, Aidoo, Mata, Wouters,
Malinovskyi, Pozuelo/Writers dk82, Trossard/Zhegrova dk82,
Ndongala/Buffel dk76 na Samatta.
Charleroi
: Penneteau, Martos, Rezaei, Benavente, Marinos, Baby, Hendrickx/Bedia
dk70, Dessoleil, Ilaimaharitra, N'Ganga/Nurio dk70 na Fall/Grange dk60.
Comments