Skip to main content

Dkt. Magufuli Azindua Kituo cha Uwezeshaji cha JWTZ



Image result for Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli(picha na mtandao)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 17 Mei, 2018 amezindua kituo cha uwekezaji cha Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kilichopo katika kikosi cha Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Mgulani (831KJ) Jijini Dar es Salaam.

Kituo hicho kina viwanda vya kushona nguo, kutengeneza maji, kukereza vyuma na pia kina chuo cha ufundi stadi (VETA), shule ya sekondari Jitegemee na kumbi mbili za mikutano (Muhuga Hall na Isamuhyo Hall). Uwekezaji wote umegharimu Shilingi Bilioni 5 na Milioni 793.

Pamoja na kuzindua kituo hicho Mhe. Rais Magufuli ametembelea kiwanda cha ushonaji wa nguo kilichogharimu Shilingi Milioni 810 na ambacho kina uwezo wa kushona jozi 500 za sare za askari kwa siku na kuzalisha ajira za watu 350, na pia ametembelea kiwanda cha kutengeneza maji ambacho kimegharimu Shilingi Bilioni 1 na Milioni 600 na kina uwezo wa kuzalisha chupa 3,600 za maji kwa saa.

Akizungumza katika mkutano uliohudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Mawaziri, Makatibu Wakuu, Maafisa Wakuu na Askari wa JWTZ, Wakuu wa Majeshi wastaafu na Majenerali wastaafu, Mhe. Rais Magufuli ameipongeza JWTZ kupitia Shirika lake la SUMAJKT kwa kuitikia vizuri wito wake wa kujenga viwanda na ameahidi kuwa Serikali itaendelea kutoa ushirikiano mkubwa kwa JWTZ katika jukumu hili la kujenga uchumi wa nchi kupitia viwanda na shughuli nyingine za uzalishaji mali.

“Naomba nimpongeze Meja Jenerali Mstaafu Michael Isamuyo kwa jitihada alizozifanya kujenga miradi hii akiwa Mkuu wa JKT, nampongeza Mkuu wa JKT wa sasa na SUMAJKT kwa kazi nzuri mnayoifanya, kwa kweli leo nimefurahi sana kuona jeshi letu linajenga viwanda, huu ni mwelekeo mzuri, askari wetu sasa watashonewa nguo kutoka hapa hapa nchini kwetu” amesema Mhe. Rais Magufuli.

Mhe. Rais Magufuli ametoa wito kwa majeshi yote nchini kununua sare kutoka viwanda vya majeshi na kwa upande wa maji ametoa wito kwa Watanzania kunywa maji ya Uhuru Peak yanayotengenezwa na SUMAJKT zikiwemo ofisi za umma, na amebainisha kuwa uwekezaji huo utasaidia JWTZ kupata mapato kwa ajili ya kujiendesha na kupunguza ukubwa wa fedha za bajeti kutoka Serikalini.

Aidha, Mhe. Rais Magufuli ametoa muda wa mwezi mmoja kwa taasisi za Serikali, taasisi binafsi na watu binafsi waliokopeshwa matrekta kupitia SUMAJKT na hawajarejesha Shilingi Bilioni 38 mpaka sasa, na taasisi za Serikali zinazodaiwa na SUMAJKT Shilingi Bilioni 3.4 kutokana na kutolipia huduma za ulinzi, kulipa madeni hayo vinginevyo vyombo vya dola viwakamate wadaiwa wote popote walipo.

“Jen. Mabeyo nimekusikia juu ya madeni mnayodai, nataka ndani ya mwezi mmoja madeni haya yawe yamelipwa, najua mkipata fedha hizi mtaweza kujenga viwanda vingine ili tuendelee kuzalisha ajira kwa Watanzania na kujenga uchumi wetu” amesisitiza Mhe. Rais Magufuli.

Mapema akitoa taarifa kwa Mhe. Rais Magufuli, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jen. Venance Salvatory Mabeyo ameishukuru Serikali kwa kuunga mkono jitihada za jeshi hilo kujenga viwanda na amemhakikishia kuwa JWTZ imedhamiria kutekeleza maagizo ya Mhe. Rais ambapo kupitia mashirika yake ya Mzinga Corporation, Nyumbu Project na SUMAJKT imekamilisha viwanda vya kuchakata nafaka vya Mlale JKT na Mafunga JKT, Kiwanda cha kuchakata kahawa cha Itende JKT na inaendelea kujenga kiwanda cha mafuta ya kula cha Kigoma.

Ameongeza kuwa JWTZ inategemea kujenga kiwanda cha chumvi katika eneo la Msindo Kilwa Masoko, na kwamba ipo tayari kushirikiana na taasisi za ndani na nje ya nchi kujenga viwanda zikiwemo mifuko ya hifadhi ya jamii ya NSSF na PPF katika mradi mkubwa wa uzalishaji wa sukari wa Mkulazi, na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) ambako wataanzisha kiwanda cha maji tiba (Intravenous Fluid).

Kwa upande wake Waziri wa Ulinzi na JKT Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema mazungumzo na nchi ya Misri yamekwenda vizuri ambapo kwa ushirikiano na JWTZ wataanzisha kiwanda cha dawa, kujenga machinjio na kiwanda cha kuchakata nyama, wakati Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage amesema kujengwa kwa kiwanda cha maji ya Uhuru Peak kunafanya Tanzania iwe na jumla ya viwanda vya maji 67 vilivyojengwa kuanzia mwaka 2015 na ambavyo vimezalishaji ajira 6,000, vimelipa kodi Shilingi Bilioni 59.7 na vimefanikiwa kutosheleza mahitaji nchini.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
17 Mei, 2018

Comments

Popular posts from this blog

MBINU ZA KUMFIKISHA MWANAMKE MWENYE MAKALIO MAKUBWA KILELENI KWA HARAKA

Kwa kawaida wanawake wanafikia kilele (mwisho wa utamu wa ngono) kati ya dakika ishirini na saa moja, yaani kwa kifupi inawachukua muda mrefu sana hali inayopelekea mpenzi mvivu kuchoka na ufanyaji wake utakuwa wa “ovyo” hali itakayo kufanya wewe kuishiwa na hamu ya kuendelea. Pamoja na kuchelewa huko ambako kunatokana na utofauti wetu kati ya mwanaume na mwanamke lakini nakumbuka hapo nyuma nilikutana na wanawake 2 waliokuwa ndani ya ndoa na wamezaa lakini hawajawahi kabisa kujua utamu wa tendo hilo alimaharufu kama “kufanya mapenzi”. Natambua kuwa ni ngumu au niseme si wanawake wote ambao wamejaaliwa kimaumbile kwamba wanafanikiwa kufika kileleni zaidi ya mara mbili kila wanapofanya mapenzi/ngono (kumbuka ni kati ya dakika 15 na saa moja hivyo Jibaba hapa awe na uwezo wa kujizuia kwa zaidi ya dk 45) na ikiwa jamaa ni “mzamiaji” basi unaweza ukaondoka na goli 3 ktk mzunguuko mmoja. Lakini kwa nini basi baadhi yao tu ndio wafike kileleni na wengine was...

Mushikiwabo to UN: Enhance civilian protection

By Eugene Kwibuka Rwanda’s Minister of Foreign Affairs and Cooperation has urged the United Nations Security Council (UNSC) to invest more energy in the prevention of conflicts for better protection of civilians living in conflict-torn areas. Rwanda’s Foreign minister, Louise Mushikiwabo Louise Mushikiwabo made the call during an open debate on the protection of civilians in armed conflict which the UNSC held in New York on Tuesday. “Rwanda’s core message today is that enhancing the protection of civilians in armed conflict requires action before a conflict starts. The proliferation of non-state armed groups makes civilian protection both more urgent, and harder to achieve,” she said. For better protection of civilians in armed-conflict areas, the minister emphasised the need to increase investments in professionalising the military and police forces through adequate training. “Only when the leadership of armed forces shares the international...

Saudi King urges U.N. action against religious insults

Saudi King Abdullah urged the United Nations to produce a resolution condemning insults on monotheistic religions after the anti-Islam film in the U.S. that sparked deadly protests in many Muslim countries last month. (AFP) By AFP, MINA/SAUDI ARABIA Saudi King Abdullah on Saturday demanded a U.N. resolution condemning insults on monotheistic religions after a low-budget film produced in the U.S. sparked deadly protests last month. “I demand a U.N. resolution that condemns any country or group that insults religions and prophets,” he said during a meeting at his palace with religious figures and heads of hajj delegations in the Mina valley where pilgrims were performing final rituals of hajj. “It is our duty and that of every Muslim to protect Islam and defend the prophets.” A low-budget film produced in the U.S., Innocence of Muslims, triggered a wave of deadly anti-American violence last month across the Muslim world targeting US symbols ranging ...