Teddy Sheringham amesema Marcus Rashford anapaswa kujinasua kwenye mikono ya Jose Mourinho kama kweli anataka kuokoa kipaji chake.
Rashaford mshambuliaji wa Manchester United mwenye umri wa miaka 20, amejikuta akiwa na nafasi finyu ya kuanzishwa kwenye mechi za United tangu Alexis Sanchez alipotua Old Trafford mwezi Januari.
Katika michezo 18 tangu ujio wa Sanchez, Rashford ameanzishwa katika michezo minne tu.
Na hapo ndipo Sheringham – gwiji wa zamani wa Manchester United, anapoona kuwa ni wakati muafaka Rashford kusaka klabu nyingine.
Comments