Benki ya CRDB yapunguza riba hadi 16% na kuongeza muda wa kulipa mkopo hadi miaka 7 kwa mikopo ya Wafanyakazi
Benki ya CRDB imeanzisha utaratibu wa kununua mikopo kwa wateja
ambao wamekopa katika taasisi na benki nyingine kuwapa fursa
ya kukopa katika Benki yao pendwa ya CRDB ambapo mikopo hiyo
itatolewa ndani ya siku moja kupitia matawi husika.
Wafanyakazi wenye mikopo Benki ya CRDB watapewa TemboCard Visa
Gold,Wafanyakazi pia wana fursa ya kupata kadi za mkopo za
“TemboCard World Reward” na “TemboCard Gold Credit” ambazo
huwezesha kupata mkopo bila riba.
Akizungumza katika mkutano wake na Waandishi Wahabari Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya hiyo Dokta Charles Kimei alisema Benki ya
wametangaza punguzo la riba kwa mikopo ya wafanyakazi kutoka
asilimia 22 hadi asilimia 16 na kuifanya mikopo ya wafanyakazi
Benki ya CRDB kuwa na riba ndogo zaidi katika soko.
Alisema benki hiyo imeamua kupunguza riba ili kutoa unafuu na
kurahisisha upatikanaji wa mikopo kwa wateja wake na Watanzania
kwa ujumla jambo litakalo saidia kuchochea kukua kwa uchumi wa
mtu mmoja mmoja na taifa zima kwa ujumla.
“Riba katika mikopo imekuwa kilio cha muda mrefu kwa wateja hivyo
kupelekea wengi wao kuogopa kukopa, leo hii ninafuraha kuwatangazia
kuwa kile kilio cha muda mrefu sasa tumekipatia suluhisho kwa kupunguza
riba kwa mikopo ya wafanyakazi kutoka asilimia 22 iliyokuwa ikitozwa
hapo awali hadi kufikia asilimia 16%”, alisema Dokta Kimei.
Dokta Kimei alisema mbali na kupunguza riba inayotozwa kwa mikopo, Benki
hiyo pia imefanya maboresho yafuatayo;Kiwango cha kukopa kimeongezwa
kutoka shilingi milioni 50 hadi kufikia shilingi milioni 100 ambapo muda wa mkopo
umeongezeka kutoka miezi 60 yaani miaka 5 mpaka kufikia miezi 84 ambayo ni
sawa na miaka 7.
Dokta Kimei alisema punguzo hilo la riba litakwenda kuwanufaisha watumishi
wote Serikali, mashirika na kampuni binafsi, huku akitanabaisha kuwa kiwango
cha chini cha mshahara kupata mkopo ni shilingi laki 2.
CRDB imejipambanua kuwa kwa punguzo hilo la riba litakwenda kuwanufaisha watumishi wote
Serikali, mashirika na kampuni binafsi, huku akitanabaisha kuwa kiwango cha chini
cha mshahara kupata mkopo ni shilingi laki 2.
Akizungumzia juu ya faida ya kupungua kwa riba ya mkopo, Dokta Kimei alisema hatua hiyo
itakwenda kuongeza mzunguko wa fedha kutokana na kupungua kwa gharama ya mikopo na hivyo
kuchochea kukua kwa uchumi.
Naye Farida Mbwana ambaye faida nyengine ni pamoja na kuongeza kiwango cha ukopeshaji
hivyo kuongeza kipato na mitaji ili kuchochea shughuli za maendeleo na kusema kuwa
huduma yao mpya ya Jiachie hadi miaka saba imesababisha wateja wengi kujitokeza.
Hata hivyo CRDB imeiomba Benki Kuu pamoja na Tume ya Ushindani nchini (FCC)
kufuatilia kwa karibu baadhi ya Benki ambazo zimekuwa zikiwakandamiza wafanyakazi
kwa kuwawekea vigezo na masharti magumu hasa pale wanapotaka kuhama kwenda Benki
nyengine yenye masharti na riba nafuu.
Comments