Haki miliki ya picha
Ikulu, Tanzania Rais wa Tanzania
Dkt. John Pombe Magufuli amesema serikali ya nchi hiyo haiwezi kutoa
mikopo ya kimasomo kwa wanafunzi wote wa vyuo vikuu nchini humo.
Kiongozi
huyo alisema serikali yake imekuwa ikiongeza fedha za mikopo na
kuwakopesha wanafunzi wengi zaidi lakini akasisitiza kuwa sasa haitaweza
kutoa mikopo kwa wanafunzi wote wa vyuo vikuu.
"Nataka
niwahakikishie Serikali ya Awamu ya Tano inawapenda wanafunzi wa vyuo
vikuu, lakini lazima niwaambie ukweli Serikali haiwezi kutoa mikopo kwa
wanafunzi wote" alisema.
Dkt Magufuli alisema hayo alipokutana na
wanafunzi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa (MUCE) kilichopo
katika Manispaa ya Iringa ambapo alisikiliza kero zao mbalimbali
zikiwemo zinazohusu mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu na mazingira ya
kusomea, kwa mujibu wa taarifa kutoka ikulu.Source BBC.
Comments