Katika juhudi za kukuza uwekezaji hapa nchini, kituo cha uwekezaji Tanzania (TIC) ndani ya miezi minne kimefanikiwa kuandikisha miradi mipya 109 ambayo inatarajia kuwekeza mitaji ya kiasi cha dolla za kimarekani zaidi ya millioni 13 na kuajiri wafanyakazi 18, 172.
Pichani Mkurugenzi Kituo cha uwekezaji nchini Geoffrey Mwambe akizungumza na waandishi wa habari
Akizungumza jijini Dar es salaam jana Mkurugenzi Mtendaji wa kituo hicho Geoffrey Mwambe amesema kuwa miradi hiyo imewekezwa zaidi kwenye sekta za ujenzi, viwanda, usafirishaji, kilimo na miundombinu ambapo alimia 34.86 inamilikiwa na wageni, 2.75 ni ya ubia na 62.40 inamilikiwa na Watanzania.
Aidha Mwambe amewataka wakuu wa mikoa pamoja na wakuu wa wilaya na taasisi mbalimbali za kiserikali kukuza mazingira wezeshi ya uwekezaji ikiwemo kutenga maeneo ya kuwekeza.
Amesisitiza wakuu wa mikoa , kufanya tasmini ya mara kwa mara ya kuhusiana na uwekezaji katika mikoa yao, ambapo amewataka kutowanyanyasa wawekezaji na kuboresha mazingira wezeshi kwa wafanyabiasha.
Amesema kuwa juhudi hizo kizifanyika kwa nguvu na msisitizo mkubwa kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa sekta hiyo, kutawezesha kukuza uwekezaji nchini na kuibua fursa kubwa za ajira kwa vijana.
Alisisitiza kuwa endapo Serikali pamoja na taasisi mbalimbali zitaweka jitihada kubwa katika kuwekeza kwenye sekta ya viwanda kutasaidia kupanua wigo wa walipa kodi, na hatimaye kuongeza uzalishaji na kufikia uchumi wa kati.
Aidha alizitaka taasisi zote nchini pamoja na mamlaka zote husika kukuza ushirikiano na kituo hicho cha uwekezaji kuweza kujenga huelewa na kutoa miongozo ili kuweza kusimamia ujenzi wa viwanda nchini.
Pia Mkurugenzi huyo alisema kuwa kituo chake kimeongeza ofisi nne mpya za kanda katika mikoa ya Dodoma, Dar es salaam, Mtwara na kigoma ambazo ni kanda ya kati, wakati kanda ya mashariki vituo vilivyoongezwa ni pamoja na pwani na Dar es salaam.
"Uboresha wa huduma katika kituo cha uwekezaji unasaidiwa zaidi na mfumo uitwao (one stop facilitation Center) ndani ya ofisi zetu ambapo mfumo huo hutoa huduma za usajili wa makampuni pamoja na kodi" alisema Mwambe.
Hata hivyo kituo hicho kinashirikiana na Serikali katika kutoa ushauri na kuboresha mazingira ya uwekezaji ambapo kulingana na Takwimu za Benki ya Rand Merchant(RMB) zilizotolewa mwaka 2015, Tanzania ilishika nafasi ya Tisa kati ya nchi kumi zenye ushawishi wa kuvutia wawekKakuwekeza.
Comments