MKURUGENZI Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Bw. Geoffrey Mwambe amefanya ziara ya kikazi nchini Ujerumani na Uholanzi kati ya Mei 14 na 17 mwaka huu katika jitihada zake za kutangaza fursa za uwekezaji ili kushawishi na kuvutia wawekezaji kuja kuwekeza nchini. Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania Bw. Geoffrey Mwambe (kulia) alipomtembelea Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Mhe. Dkt. Possi Abdallah ofisini kwake Berlin, Ujeruman Akiwa nchini Ujerumani Bw. Mwambe alisema lipokelewa na Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Mhe. Dkt. Possi Abdallah ambapo walifanya kikao cha kazi kabla ya kushiriki kongamano la biashara na uwekezaji kati ya Ujerumani na nchi za Afrika Mashariki lililofanyika Mei 15, 2018 katika mji wa Berlin. Pichani baada ya kukamilisha zoezi la kusaini MOC . waliokaa kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa TIC Bw. Geoffrey Mwambe na kushoto n...