Makamu wa rais Joseph Boakai akubali kushindwa Liberia J Makamu wa rais waLiberia Joseph Nyuma Boakai ampongeza George Weah kwa ushindi wake Desemba 29, 2017 katika hotuba alioitoa Monrovia, mji mkuu wa Liberia Siku moja baada ya tume ya uchaguzi nchini Liberia NEC kumtangaza nyota wa zamani wa Soka, George Weah, mshindi wa duru ya pili ya uchaguzi wa urais nchini humo, makamu wa rais Joseph Nyuma Boakai amekubali kushindwa na kumpongeza mpizani wake. George Weah alishinda kwa 61.5% ya kura , huku mpinzani wake, Makamu wa rais Joseph Boakai akipata 38.5% , Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ilitangaza. Weah atachukua nafasi ya Ellen Johnson Sirleaf ambaye alikuwa rais wa kwanza mwanamke barani Afrika kuchaguliwa kidemokrasia na sasa anatarajiwa kukabidhi madaraka kwa amani. Rais Sirleaf alimshinda Weah katika uchaguzi wa duru ya pili uliofanyika mwaka 2005, baada ya kumalizika kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa miongo kadhaa nchini humo. Punde baada ya...