MSANII kutoka katika kundi la Wateule Jafari Mshamu aka Jahffaray amesma kuwa kwa sasa amesitisha kutoa albamu ambapo atakuwa akitoa wimbo tu . Akizungumza usiku sikuchache zilizopita kwenye ukumbi wa Nyumbani Lounge Dar es Salaam Jafari alisema kuwa , kutoa wimbo na kusambaza msanii anapata faida mapema kupitia maonesho katika mialiko. "Kwa sasa nimesitisha kuipua albamu kwani, maandalizi yaeke yanatumia muda mrefu , uku utoaji wa wimbo ni wa muda mfupi na unaingiza kwa haraka kipato cha msanii,"alisema. Tayari msanii huyo anatarajia kuachia nyimbo mbili zinazoitwa ‘Tembea na mimi’ na ‘Amsha Amsha', ambapo amesisitza kuacha kabisa kwa yeye kutoa albamu.