Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Makamu
wa Rais (Mazingira) Dk Terezya Huvisa, amemtuhumu Katibu Mkuu wa wizara
moja (anahifadhiwa) kwa kumkingia kifua Robert Mugishagwe anayemiliki
isivyo halali kiwanja namba 2002 kilichoko Kawe Beach, jijini Dar es
Salaam.Akijibu maswali ya wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Ardhi,
Maliasili na Mazingira iliyotembelea Baraza la Taifa la Mazingira jana,
Dk Huvisa alisema hamwogopi mtu yeyote kwa sababu anasimamia sheria.
Comments