Na Sargajan bin Kadii, Nairobi
Wanachama wa makundi mawili pinzani ambayo yametisha wakaazi na Wasomali
wanaomiliki biashara katika kitongoji cha Eastleigh mjini Nairobi kwa
miaka mitatu iliyopita wako katika kukimbiakimbia baada ya kuchukuliwa
kwa hatua kali za usalama, maofisa wa eneo hilo walisema.
Kijana asiye wa kabila wa Kisomali
akijiandaa kupambana kwa mawe katika makabiliano ya tarehe 19 Novemba,
2012 wakati wa mapambano ya kulipiza kisasi dhidi ya kabila la Wasomali
ambayo yalitokea huko Eastleigh baada ya mlipuko wa bomu uliodaiwa
kufanywa na al-Shabaab na kuua na kujeruhi watu kadhaa. Wakati wa
mapambano hayo, makundi pinzani ya Wasomali yaliungana kulinda maslahi
ya Wasomali [Tony Karumba/AFP]
Makundi hayo mawili, yanayojulikana kama Superpower na Sitaki Kujua (SK) yanajumuisha hasa Wasomali.
"Tayari tumeshawakamata wanachama zaidi ya 500 wa makundi hayo," alisema
Ndumba Thangalani, ofisa wa uchunguzi wa uhalifu wa wilaya ya Starehe,
ambapo Eastleigh iko huko.
Mwishoni mwa mwezi Julai, operesheni ya polisi iliwakamata wanachama 51,
wengi wao walishtakiwa mahakamani na kuachiwa baada ya kulipa dhamana
ya fedha taslimu ya shilingi milioni moja (dola 11,400) kila mmoja,
aliiambia Sabahi. Wale walioshindwa kulipa waliwekwa rumande na
wanasubiri hukumu.
"Kwa kuwepo kwa kesi chache sana ziliripotiwa [kwa polisi wakati wa]
Ramadhani ni ishara kwamba tunashinda vita dhidi ya Superpower na SK,"
Thangalani alisema.
Baadhi ya wanachama wa kikundi ambao walikamatwa tangu mwishoni mwa 2012
baadaye walikiuka dhamana na kushindwa kufika mahakamani tarehe
walizotakiwa, lakini viongozi wametoa hati za kukamatwa kwao, alisema.
Comments