HABARI/PICHA na bongostaz.blogspot.com
BONDIA
Mtanzania, Francis ‘SMG’ Cheka usiku wa kuamkia leo ametawazwa kuwa
bingwa mpya wa dunia wa WBF, katika uzito wa Super Middle baada ya
kumshinda Mmarekani, Phil Williams kwa pointi katika pambano la Raundi
12, lililofanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam.
Jaji
wa kwanza Eddie Marshall kutoka Afrika Kusini alitoa pointi 116 kwa
115, jaji wa pili Fidel Hayness alitoa pointi 119 kwa 118 na jaji wa
tatu, John Chagu alitoa pointi 117 kwa 116 (wote wa Tanzania), wakimpa
ushindi Cheka.
Kwa ushindi huo, Cheka amefuata nyayo za bondia
mwingine Mtanzania, Rodgers ‘Tiger’ Mtagwa ambaye aliwapiga Wamarekani
kadhaa kwao, ambako anaishi tangu 1998.
|
Bondia
Francis Cheka wa Tanzania akimtupia konde Mmarekani, Phil Williams
katika pambano la Raundi 12 kuwania ubingwa wa dunia uzito wa Super
Middle usiku huu ukumbi wa Diamond Jubilee kuwania taji la WBF. Cheka
ameshinda kwa pointi.
|
|
Thomas Mashali kulia ameshinda kwa pointi dhidi ya Mada Maugo
Miongoni
mwa mabondia Wamarekani ambao Mtagwa, mtoto wa Keko Mwanga, Temeke, Dar
es Salaam amewahi kuwapiga ni Garvin Crout kwa Knockout (KO) Raundi ya
kwanza pambano la Raundi nane, kwenye ukumbi wa Blue Horizon,
Philadelphia, Pennsylvania, Marekani pambano lililochezeshwa na refa
James Condon Septemba 12, mwaka 2000 na mwingine Donovan Carey kwa KO
pia Raundi ya Pili Juni 15, 2001 ukumbi huo huo.
Katika
pambano hilo lililochezeshwa na refa kutoka Afrika Kusini, Drake
Ribbinck, mabondia hao walianza kwa kusomana Raundi ya kwanza
wakitupiana makonde ya tahadhari na katika Raundi ya pili, kila mmoja
alitaka kuhakikisha kile alichogundua kwa mpinzani wake kabla ya kazi
kuanza Raundi ya Tatu.
Cheka
aling’ara katika Raundi ya Tatu na ya nne na Mmarekani akaibuka Raundi
ya Tano na kuanza kuonyesha upinzani. Raundi ya Sita Mmarekani aliongeza
kasi ya urushaji makonde na Raundi ya saba na ya nane walipigana sawa,
ingawa Williams alianguka kwa kuteleza na kuinuka kuendelea na pambano.
Raundi
ya 10 mabondia hao waliendelea kutupiana makonde kwa zamu, lakini
Raundi ya 11 na 12 pamoja na Williams kusimama imara kutafuta ushindi wa
Knockout (KO), lakini SMG alikuwa makini katika kukwepa na kurusha
ngumi za kudonoa kichwani kwa mpinzani wake.
Na kwa sababu hiyo haikushangaza baada ya pambano, bondia mwenye maskani yake Morogoro kutangazwa bingwa mpya wa WBF.
Waziri
wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo, Dk Fenella Mukangara aliyekuwa
mgeni rasmi alijaribu kwa tabu tabu kumvisha taji Cheka kutokana ulingo
kuvamiwa na mashabiki waliopagawa na ushindi wa bondia huyo.
Katika
mapambano ya utangulizi, Thomas Mashali alimshinda kwa pointi Mada
Maugo, wakati Alphonce Mchumia Tumbo alimshinda kwa Technincal Knockout
(TKO), baada ya wasaidizi wake kurusha taulo Raundi ya tano katika
pambano la Raundi sita.
Hata
hivyo, dosari iliyojitokeza katika usiku huo ni mabondia kugoma
kupanda ulingoni hadi kwanza walipwe fedha zao na ilianzia kwa Mchumia
Tumbo, ikafuatia kwa Maugo na Mashali na baadaye Cheka.
Bingwa
wa zamani wa dunia, bondia wa Afrika Kusini, Francois Botha alilaani
hali hiyo na kusema mabondia wanapanda ulingoni kwa ajili ya fedha,
hivyo kutokokuwa na uhakika wa malipo yao si sawa.
Alipoulizwa
kuhusu malipo yake, Botha aliyewahi kupigwa kwa mbinde na bingwa wa
zamani wa dunia, Mmarekani, Mike Tyson alisema yeye amekuja kwa mradi
maalum wa kampeni kuzuia Malaria na hana anachodai kwa waandaaji wa
pambano hilo.
|
Comments