Muungano umeendelea kuumiza vichwa ambapo mkoani Mwanza wajumbe wamevutana kiasi cha kumtia majaribuni mwenyekiti wa baraza
Mwanza. Wajumbe wa Baraza la Katiba wilayani Nyamagana, wamechafua hali
ya hewa na kumweka mwenyekiti wa baraza hilo, Muhamed Mshamba katika
wakati mgumu baada ya kuibuka makundi mawili yaliyokuwa yakivutana
kuhusu Muundo wa Muungano.
Wakati kundi moja likiwa linatetea Muundo wa Serikali mbili, lingine
likataka Serikali tatu. Kundi linalotaka Serikali tatu limeeleza kuwa
Serikali mbili kufanya kazi ilizotumwa za kuwaletea wananchi maendeleo
endelevu.
Akichangia hoja hiyo, mwakilishi wa wananchi wa Kapripot, Milton
Rutabana alisema kuwa, Muungano wa Serikali mbili umeshindwa kutatua
kero nyingi, ikiwemo fursa za maendeleo katika nyanja za uchumi, siasa
na jamii.
Alisema kuwa Serikali mbili za Muungano zimekiuka makubalianao
yaliyowekwa kwenye hati ya Muungano ya mwaka 1964. “Ilitakiwa kuwa na
Muungano wa Jamhuri ya Tanganyika, Jamhuri ya watu wa Zanzibar kwa jina
la Muungano wa Tanganyika na Zanzibar,” alisema.
Aliendelea kufafanua na kudai kuwa mambo ya Muungano yalikuwa mawili tu
mwaka huo wa 1964, lakini sasa hivi yameongezeka na kufikia mambo 22
bila ya ridhaa ya wananchi kutoka pande zote mbili za Muungano.
Comments