Wanajeshi wa Misri wakiwa nje ya msikiti wa Al- Fath thehindu.com |
Na Sabina Chrispine Nabigambo
Wanajeshi wa Misri leo Jumamosi wameingia ndani ya msikiti wa Al-Fath
jijini Cairo ambako waandamanaji wa kiislamu wamejikusanya kwa usiku
mzima siku moja baada ya mapigano ya umwagaji damu kushuhudiwa nchini
humo
Picha za moja kwa moja za kituo binafsi cha televisheni nchini humo ONTV
zimewaonesha wanajeshi hao wakifanya majadiliano na waandamanaji
kujaribu kuwashawishi kuondoka msikitini hapo.
Mmoja wa waandamanaji aliyekuwa ndani ya msikiti huo ameliambia shirika
la habari la Ufaransa kuwa wamewataka kutowakamata na kuacha
washambuliwe na raia wenye hasira waliopo nje ya msikiti huo.
Vikosi vya usalama nchini Misri mapema hii leo vimeuzunguka msikiti wa
Al- Fath uliofurika wafuasi wa kiongozi aliyeondolewa madarakani na
jeshi Mohammed Morsi wafuasi ambao wamepanga maandamano mapya baada ya
mapigano yaliyosababisha vifo vya watu zaidi ya themanini.
Machafuko hayo yamewagawa wamisri kinyume na ambavyo imewahi kutokea
katika historia ya taifa hilo hivi karibuni,wakitofautiana na serikali
iliyowekwa madarakani na jeshi pamoja na ushawishi wa mataifa ya kigeni.
Chanzo - kiswahili.rfi.fr
Comments