Brigette
Alfred pamoja na baadhi ya wanafunzi walemavu wa ngozi wa shule ya
msingi Buhangija wakinyanyua moja kati ya mabati 200 aliyonunua kwa
ajili ya ujenzi wa bweni la wavulana katika shule hiyo,CHANZO:Majuto
Omary.
Na Mwandishi wetu, Shinyanga
MREMBO wa
Tanzania, Brigitte Alfred ameonyesha mfano wa kuigwa nchini katika
tasnia hiyo baada ya kuanza ujenzi wa bweni la wanafunzi wenye ulemavu
wa ngozi (albino) katika wilaya ya Shinyanga wanaoishi katika shule
maalum ya Buhangija.
Tayari
mrembo ameweka jiwe la msingi na kupandisha ukuta sambamba na kukabidhi
mabati 200 kwa ajili ya kujengea paa la bweni hilo la wavulana lenye
uwezo wa kulaza wanafunzi 50.
Makabidhiano
hayo yalifanywa na mrembo huyo kwa katika hafla fupi iliyohudhuriwa na
mkuu wa wilaya ya Shinyanga Annarose Nyamubi, afisa elimu wa manispaa ya
Shinyanga Honoratha Ruhumbika na walimu wa shule hiyo wakiongozwa na
mwalimu mkuu, Peter Ajali.
Briggite
alisema kuwa ameamua kutimiza ahadi yake aliyoitoa mwezi Aprili mwaka
huu alipotembelea Shinyanga kwa kazi za jamii na kuona changamoto za
watoto wanaosoma katika shule hiyo.
Alisema
kuwa mpango huo upo katika mpango wa Miss Tanzania ujulikano kwa jina la
Urembo wenye malengo maalum (Beauty with Purpose) nay eye kuamua
kufanya kwa vitendo.
"Ni
faraja kwangu kuona kuwa ninatimiza ahadi yangu, nawashukuru wote
walionisaidia ikiwa pamoja na familia yangu, na ninaomba wengine
wanisaidie kwani badi kuna changamoto nyingi katika ujenzi na kazi za
jamii kwa ujumla," alisema Brigitte.
Alisema
kuwa amepania kuweka historia katika fani hiyo kwani anaamini ujenzi au
jingo hilo litakuwa kumbukumbu kubwa kwake tena kwa vizazi na vizazi.
Brigitte
pia aliwataka wanafunzi hao kutokata tamaa hata kwa wale wasiokuwa
karibu na familia zao na kwamba wamtegemee zaidi Mwenyezi Mungu kwa kuwa
yeye ndiye mfariji kwa wanyonge huku akiwahimiza kuzingatia zaidi elimu
kwani ndiyo msingi wa maisha yao.
"Nilipata
msukumo wa kuisaidia shule hii hususani katika ujenzi wa bweni hilo
kutokana na ujio wake wa mwezi Aprili mwaka huu shuleni hapo na kujionea
adha wanayopata watoto hao kutokana na msongamano mkubwa mabwenini,"
alisema.
Mkuu wa
wilaya ya Shinyanga Annarose Nyamubi alimpongeza Brigitte kwa moyo huo
wa kujitolea na kuwataka warembo wengine kuiga mfano wake.
Nyamubi
alisema kuwa alichokifanya Brigitte ni jambo la kukumbukwa nan i msaada
mkubwa kwa jamii hasa kwa watu wenye ulemabu wa ngozi.
Mkuu huyo
wa wilaya aliwaomba wazazi wa watoto hao kuwa na tabia ya kuwatembelea
watoto wao mara kwa mara ikiwa ni pamoja na kuwachuku wakati wa likizo.
Naye
mwalimu mkuu wa shule hiyo Peter Ajali alisema kuwa shule hiyo
inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo la msongamano mabwenini
kwani kuna jumla ya watoto 247 huku mabweni yaliyopo yana uwezo wa kukaa
watoto 148 tu.
Comments