Rais mteule wa Zimbabwe Robert Mugabe/rfi
Rais mteule wa Zimbabwe Robert Mubage ataapishwa siku ya Jumatano ikiwa
chama cha Movement for Democratic Change hakitawasilisha kesi Mahakamani
kupinga ushindi wa Mugabe uliotanagzwa Jumapili iliyopita.
Ikiwa MDC itawasilisha kesi Mahakamani ya kupinga matokeo hayo, Mugabe atasubiri siku saba kabla ya kuapishwa.
Waziri Mkuu Morgan Tsvangirai amesema hawezi kutambua ushindi wa rais
Mugabe wa asilimia 61 kwa kile alichokisema kuwa uchaguzi huo haukuwa
huru na haki.
Waangalizi wanasema licha ya uchaguzi huo kuwa huru, tume ya uchaguzi inastahili kufanyiwa marekebisho.
Tume ya taifa ya uchaguzi nchini humo ZEC inatuhumiwa kuongeza mara
mbili zaidi karatasi za kupigia kura na kufikia milioni 8.6 badala ya
milioni 6.5 ya idadi ya watu waliojiandikisha kupiga kura
Via kiswahili.rfi.fr
Comments