Imeandikwa na Magreth Kinabo —
SERIKALI imesema kwamba operesheni ya kuwaondoa wahamiaji haramu katika
Kanda ya Ziwa itaanza kwa ghafla, huku ikiendelea kusisitiza kwamba watu
wanoaishi nchini bila taratibu za kisheria kuondoka kwa hiari na mali
zao.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dkt.
Emmanuel Nchimbi akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es
Salaam kuhusu wahamiaji haramu waliorejea kwao baada ya agizo la Rais
Jakaya Kiwete alilolitoa Julai 29, mwaka huu katika ziara yake ya mkoa
wa Kagera. (Picha na Lorietha Laurence)
Kauli hiyo imetolewa leo na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dkt.
Emmanuel Nchimbi wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu
wahamiaji haramu waliorejea kwao baada ya agizo la Rais Jakaya Kiwete
alilolitoa Julai 29, mwaka huu katika ziara yake ya mkoa wa Kagera.
“Nimeshapewa maelekezo rasmi na Rais Jakaya Kikwete ya kuwaondoa
wahamiaji haramu nitakapoona inafaa. Operesheni itaanza ghafla haiko
mbali.
Muda mwuafaka wa kutekeleza vyombo vya dola vitasema. Tunatoa wito waondoke wenyewe na mali zao bila kunyang’nywa. Wenye mali nyingi wanatakiwa kutoa taarifa katika vituo vya polisi ili waweze kusindikizwa. Hatutawavumilia wahamiaji haramu,” alisema Waziri Nchimbi.

Aliongeza kuwa wahamiaji hao wanaotaka kuishi nchini wanatakiwa kurudi
nchini kwao kwanza na kufuata taratibu za kisheria kama ambavyo nchi
nyingine zinavyofanya mtu akitaka kuishi nchi yoyote anatakiwa kufuata
taratibu hizo.
Comments