Polisi ya Kenya imetahadharisha kuwa kundi la kigaidi la al Qaida
linajitayarisha kufanya mashambulizi katika mji wa pwani wa Mombasa
katika kumbukumbu ya mauaji ya msomi wa Kiislamu Sheikh Aboud Rogo.
Taarifa ya polisi ya Kenya ambayo hadi sasa haijamtia nguvuni mtu
aliyemuua msomi huyo wa Kiisalmu, imesema kuwa kundi la al Shabab
linaloshirikiana na mtandano wa al Qaida, huenda linapanga kufanya
mashambulizi ya kukumbuka kuuliwa msomi huyo.
Mkuu wa polisi ya kaunti ya Mombasa Robert Kitur amesema jeshi la polisi
limepata taarifa za kipelelezi kuhusu tishio la shambulizi la kundi la
al Shabab katika mji wa Mombasa katika kumbukumbu ya mauaji ya Sheikh
Aboud Rogo.
Kitur amesema usalama umeimarishwa zaidi katika mji wa Mombasa na kwamba
polisi imezuiya maandamano ya kukumbuka tukio la kuuawa Sheikh Rogo.
Waislamu wengi wa Kenya wanaituhumi serikali ya nchi hiyo kwamba
ilihusika na mauaji ya Sheikh Aboud Rogo yaliyofanyika Agousti 27 mwaka
jana. Vyombo vya usalama vya Kenya hadi sasa havijamkamata mtu au watu
waliofanya mauaji hayo.
Comments