Na Rajab Mkasaba. Ikulu
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed
Shein amezipongeza juhudi zilizochukuliwa na Jamhuri ya Kenya katika
kujiletea maendeleo ikiwa ni pamoja na kuitumia vyema demokrasia kwa
kufanya uchaguzi kwa amani na utulivu.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akizungumza na Balozi wa Kenya Nchini Tanzania Mhe,Mutinda Mutiso,alipofika Ilkulu Mjini Zanzibar kumuaga Rais,akiwa amemaliza muda wake wa kazi Nchini
Dk. Shein aliyasema hayo leo wakati alipokuwa na mazungumzo na Balozi wa
Kenya nchini Tanzania Mhe. Mutinda Mutiso aliyefika Ikulu mjini
Zanzibar kwa ajili ya kuaga baada ya kumaliza muda wake wa kazi nchini
Tanzania.
Dk. Shein alimueleza Balozi huyo kuwa mafanikio yaliopatikana kutokana
na kufanya uchaguzi wa kihistoria nchini humo uliofanyika mwezi Machi
mwaka huu, yameweza kuijenga sifa kubwa Kenya ndani na nje ya bara la
Afrika.
Alieleza kuwa Zanzibar inathamini sana uhusiano na ushirikiano wa kidugu
na wenye historia uliopo kati ya Kenya na Zanzibar hasa ikizingatiwa
kuwa nchi zote zipo katika Mwambao wa Afrika Mashariki.
Comments