Na Mwandishi Wetu
PROFESA Wamba Dia Wamba kutoka Jamhuri
ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) ameunga mkono kauli ya Rais Jakaya
Kikwete iliyozua mvutano kati ya Rais wa Rwanda Paul Kagame na Tanzania,
na kudai kikwete yuko sahihi.
Profesa Wamba mtaalamu wa historia aliunga mkono kauli ya Rais Kikwete alipokuwa akifanya mazungumzo na baadhi ya wadau wa Mtandao wa Wanabidii waliomtembelea nyumbani kwake nchini Tanzania na kuzungumza naye masuala anuai ya Afrika.
Profesa Wamba mtaalamu wa historia aliunga mkono kauli ya Rais Kikwete alipokuwa akifanya mazungumzo na baadhi ya wadau wa Mtandao wa Wanabidii waliomtembelea nyumbani kwake nchini Tanzania na kuzungumza naye masuala anuai ya Afrika.
Katika mazungumzo yake Prof. Wamba
alisema Rais Kikwete yuko sahihi kwa kauli yake aliyoitoa hivi karibuni
mkutanoni akimshauri Rais wa Rwanda kukaa na kuzungumza na makundi
anayovutana nayo nchini kwake ya Interahamwe na FDLR ili kumaliza
mvutano.
"Mi nadhani Rais Kikwete yupo sahihi
kumshauri Rais Kagame kwamba wakae na kufanya mazungumzo ili kumaliza
mzozo...na pia kauli hiyo hakuitoa kwa Kagame pekee bali na viongozi
wengine wa nchi zikiwemo Uganda, DRC na Rwanda yenyewe, mbona hawa
hawakuzua uhasama huo," alisema Prof. Dia Wamba.
Rais Kagame amekuwa akitoa kauli ya
kejeli vitisho kwa Tanzania na Rais Kikwete tangu kutoka kwa kauli ya
kumshauri kufanya mazungumzo na makundi wapinzani wake ya Interahamwe na
FDLR.
Akizungumzia mgogoro wa DRC Profesa
huyo alisema unasababishwa na hila za kimaslahi dhidi ya pande
mbalimbali, yakiwemo baadhi ya mataifa ya kimagharibi hasa kwenye madini
yanayopatikana eneo hilo. Akizungumzia mtanzamo wa jumla kwa nchi za
Afrika kiongozi huyo alisema anashangaa kuona mambo ambayo awali
yalikuwa yakipingwa dhidi ya utawala wa kikoloni yanafanywa sasa na
baadhi ya viongozi wa mataifa ya kiafrika tena kwa kiwango kikubwa
tofauti na awali
ilhali nchi hizo zipo huru. Aliongeza
vitendo vya rushwa, ubinafsi, ubaguzi na matumizi mabaya ya rasilimali
za umma bado ni changamoto kwa mataifa mengi ya Afrika na ndiyo vikwazo
kwa maendeleo ya wananchi wa nchi hizo.
*Imeandaliwa na www.thehabari.com
Comments