Na Deodatus Balile, Dar es Salaam
Mauaji ya watu yanayofanywa na mamlaka za serikali pasipo kufuata sheria pamoja na vurugu zinazohusiana na makundi na uchawi vimegharimu maisha ya mamia ya Watanzania katika kipindi cha kwanza cha 2013, kwa mujibu wa ripoti ya hivi karibuni ya Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) jijini Dar es Salaam.
Josephine Slaa, mke wa mpiga kampeni dhidi ya rushwa na mgombea urais William Slaa, anasaidiwa kuingia katika gari la polisi baada ya kupigwa na polisi waliokuwa wakipambana na ghasia wakati wa maandamano ya chama cha upinzani tarehe 5 Januari, 2011. Ripoti mpya iliyotolewa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu imesema mapambano baina ya raia na vikosi vya usalama vya taifa yamesababisha raia 22 na maofisa polisi 8 kufariki dunia katika nusu ya kwanza ya 2013. [Stringer/AFP]
Wakati baadhi ya viashirio vinaonyesha kuboreka kwa kiasi ikilinganishwa na miezi sita ya kwanza mwaka uliopita, matokeo ya jumla ya kituo hicho yameibua wasiwasi kwamba Watanzania wanajichukulia sheria mikononi na kupuuza sheria iliyopo.
Vurugu za vikundi zilisababisha mauaji ya watu 597 katika kipindi cha nusu ya kwanza ya mwaka huu, ikiwa ni ongezeko kutoka vifo 563 kati ya Januari na Juni 2012, LHRC ilisema katika taarifa yake ya nusu mwaka iliyotolewa tarehe 29 Julai. Watu wengi kadri ya 303 waliuawa katika vurugu zilizohusiana na uchawi katika kipindi cha miezi sita ya kwanza ya 2013, ikipungua kutoka 336 katika kipindi kama hicho cha mwaka uliopita.
Katika vurugu za kuua ambazo zilitokea kipindi cha miezi sita ya mwanzo ya mwaka huu, polisi wa Tanzania, wanamgambo na vikosi vya jeshi waliwaua raia 22, ambapo raia waliwaua polisi wanane wakiwa kazini, LHRC iliripoti.
"Mwaka uliopita, watu 31 waliuawa katika mauaji yaliyofanywa na vyombo vya serikali pasipo kuzingatia sheria mwaka mzima" Mwansheria na mtafiti wa LHRC Pasience Mlowe aliiambia Sabahi. "Miezi sita ya mwaka huu, tayari watu 22 wameshauawa. Kiwango kinaidaiwa kuongezeka."
Comments