Skip to main content

MANAIKI SANGA(MANEY IS PAPER ) ATIWA MBARONI KWA KUPIGA PICHA ZA UTUPU NA WATOTO WADOGO



Jeshi la polisi kanda ya Dar es Salaam linadaiwa kumtia mbaroni msanii anaetuhumiwa kupiga picha chafu na wanawake mchanganyiko wakiwema mamiss maarufu na baadae kusambaza kwenye mitandao yote ya kijamii pamoja na kuripotiwa kwenye magazeti pendwa. 


Gazeti hili katika upekenyuaji wake limenasa picha hizi kwenye mtandao mmoja maarufu wa kijamii ukimuonesha Manaiki akiwa kwenye kibano kikali cha polisi huku akiwa amevishwa pingu na kurukishwa kichurachura.

Habari za uhakika  zinasema kuwa msanii huyo aliyeshiriki kwenye filamu za Tikisa, Love Position, Last Coin na Sory my Soni alikamatwa siku chache baada kuvuja kwa picha zake za aibu zikimuonesha akiwa na wanawake tofauti tofauti.

Aidha picha zaidi za tukio hilo la kukamatwa kwa Manaiki na haikufahamika kama alikamatwa kwa kosa jingine tofauti na kosa la kudhalilisha wanawake ambapo hali hiyo iliwalazimu waandishi wetu kufatilia kwa ukaribu tukio hilo la kukamtwa kwa msanii huyo aliyejitapia usataa kwa matukio ya picha za uchi .

Timu ya waandishi wetu ilifika kituo cha Polisi Buguruni kwa ajili ya kufahamu kama msanii huyo alikuwa ameswekwa kituoni hapo lakini kwa bahati mbaya hakuwepo. Ambapo gari la mapapalazi weti ilielekezwa kituo cha Polisi Oysterbay kwa ajili ya kuonana na RPC wa Kanda ya Kinondoni Wambura lakini pia kwa bahati mbaya mara baada ya kufika ofisini kwake sekritali wake alisema kamanda hakuwepo kwa muda huo.

Alipotafutwa msanii huyo kupitia simu yake ya kiganjani ili kujuwa nini kilimsibu lakini hakuweza kupatikana kwani simu yake ilikuwa haipatikani kabisa licha kupigwa zaidi ya mara sita.


Aidha kukamatwa kwa Manaiki kumeleta tafsiri tofauti kuwa huenda Rais wa Miss Utalii Tanzania Gidion Chipungahelo anahusika kufuatia kauri yake aliyoitoa kwenye la Kiu la wiki iliyopita kuwa lazima ataanza kumshughulikia Manaiki ili iwe fundisho kwa wale wote wanaosubiri kuwafanyia skendo chafu warembo wake. Hata hivyo licha waandishi wetu kufatilia habari hiyo karibu siku nzima lakini hapakuwa na taarifa sahihi za wapi alipo Manaiki na kituo gani cha Polisi alichoswekwa ambapo  juhudi nyingine za kufika nyumbani kwa msanii huyo na baadae tutawaletea taarifa kamili.

WAZAZI WATOA KAURI NZITO: 
Baada ya wiki iliyopita tumepokea maoni mbalimbali ya wananchi hasa wazazi wenye uchungu na wa watoto wao na walifunguka mengi sana fuatilia ujue kauri zao.

Mama Amina wa Mbezi Beach alisema “ Jamani hivi huyo msanii ana wazazi kweli? Hapana binafsi siamini kama anao kwani udhalilishaji anaoufanya kwa watoto wa watu kama angekuwa na wazazi hakika wangemkanya na angeachana na huo upuuzi nasema hii haikubariki kabisa tunamuomba Kamanda Kova amshughulikie kijana huyo ili iwe fundisho kwa wengine” Alisema mama huyo kwa uchungu

Nae Mama Mud wa Sinza Jijini Dar alifunguka hivi “ Unajua huyu Manaiki mimi ni mmoja wa mashabiki wake kwenye muziki wa bongo flava sasa nashindwa kuelewa kwa nini amejidhalilisha kwa picha chafu kama hizo? Sio bure mi nadhani anahitaji ushauri nasahaa kwani huenda sio akili yake haki ya Mungu” Alisema

Aidha nae msanii mkongwe wa tasinia ya filamu nchini Mzee Magali alitoa ushauri kwa Manaiki na kusema“ Huyu motto ana kipaji kizuri sana kwenye kuimba kuigiza sasa ni nini kinachomfanya ajidhalilishe kiasi hiki dar kweli imeuma sana kuona kijana wangu anavyopotea, Kwani sasa hivi tunahitaji kudhalisha akina mzee Chilo wapya. Akina mzee Magali wapya sasa kwa mtindo huu hakika hawa vijana hawatofika mbali na sanaa” Alisema sema kwa uchungu

Aidha nae Hemed Kavu meneja wa Club Maisha ya Dar alikuwa na haya “ Mimi nimepiga simu hapo kuwaeleza kuwa nimesikitishwa sana na tabia ya Manaiki ambapo kwenye hizo picha pia yupo mpwa wangu ambae anasema alishawishiwa na Manaiki kupiga hizo picha hivyo kama familia tutakaa chini kuangalia namna ya kumshitaki ili amradi ushahidi toka kwa muhusika upo kuwa kulikuwa na ushawishwaji wakati wa kupiga picha hizo toka kwa Manaiki ambae alimrubuni kumpa laki mbili akishapiga picha hizo” Alisema Hk

Nae mwalimu wa wasanii wengi nchini n director wa filamu Tanzania aliyejitambulisha kwa jina moja la Bakari alilonga “ Hapo mimi ninachokiona hao wote wana makosa kwani hapo hakuna mtoto mdogo hao mabint nao viherehere vyao viliwaponza hivyo kama Manaiki alifanya kwa kuwafunga kamba hapo sawa ana haki ya kuhukumiwa jamani lakini hao wanawake walijitakia wenyewe basi walaumiwe wote” Alisema.

Comments

Popular posts from this blog

Thousands of protesters clash with police in Chicago: Chaos in the Windy City as 45 activists arrested and one cop stabbed after demonstrators target NATO

By DAILY MAIL REPORTER Thousands of demonstrators upset with the war in Afghanistan, climate change and the erosion of union rights have raised the intensity of a march in downtown Chicago on Sunday as world leaders assembled for a NATO summit. The protest, one of the city's largest in years, turned violent at the end of an anti-NATO march, where demonstrators confronted Chicago police, pushing against a line of officers several blocks from the lakefront convention center where President Obama hosted a gathering of world leaders. Authorities were seen making arrests one by one and leading individual demonstrators away in handcuffs. After a clash near McCormick Place, Chicago Police Superintendent Garry McCarthy said at a news conference that the protests resulted in 45 people being arrested and four officers suffering injuries - one from a stab wound in the leg. Scroll down for video Clash: Demonstrators try to flee the police as they are move in on them ...

Mushikiwabo to UN: Enhance civilian protection

By Eugene Kwibuka Rwanda’s Minister of Foreign Affairs and Cooperation has urged the United Nations Security Council (UNSC) to invest more energy in the prevention of conflicts for better protection of civilians living in conflict-torn areas. Rwanda’s Foreign minister, Louise Mushikiwabo Louise Mushikiwabo made the call during an open debate on the protection of civilians in armed conflict which the UNSC held in New York on Tuesday. “Rwanda’s core message today is that enhancing the protection of civilians in armed conflict requires action before a conflict starts. The proliferation of non-state armed groups makes civilian protection both more urgent, and harder to achieve,” she said. For better protection of civilians in armed-conflict areas, the minister emphasised the need to increase investments in professionalising the military and police forces through adequate training. “Only when the leadership of armed forces shares the international...

Mwana muziki Marufu kwa jina la Chuck Brown Afariki Dunia Akiwa na umri wa miaka 75

View Photo Gallery — Chuck Brown dies at 75: The “godfather of go-go” has died By Chris Richards, Updated: Wednesday, May 16, 4:42 PM Chuck Brown, the gravelly voiced bandleader who capitalized on funk’s percussive pulse to create go-go, the genre of music that has soundtracked life in black Washington for more than three decades, died May 16 at the Johns Hopkins University hospital in Baltimore. He was 75. The death, from complications from sepsis, was confirmed by his manager, Tom Goldfogle. Mr. Brown had been hospitalized for pneumonia. Known as the “Godfather of Go-Go,” the performer, singer, guitarist and songwriter developed his commanding brand of funk in the mid-1970s to compete with the dominance of disco. Like a DJ blending records, Mr. Brown used nonstop percussion to stitch songs together and keep the crowd on the dance floor, resulting in marathon performances that went deep into the night. Mr. Brown said the style got its name because “the music j...