Na Mwantanga Ame, Dar es Salaam
MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi, ametaja sababu
za msingi zilizoifanya serikali kufanya marekebisho ya baadhi ya wizara
na watendaji.
Akizungumza na watendaji wa taasisi za serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
zilizopo Dar es Salaam, alisema dhamira ya serikali ni kuona kunakuwa
na uwiano katika baadhi ya wizara kiutendaji na kuongeza ufanisi.
Kutokanana hali hiyo,aliwataka watumishi kuyapokea mabadiliko hayo kama ni sehemu ya kuleta mafanikio.
Alisema natambua kuna changamoto ndani ya taasisi hizo na serikali
itajitahidi kuona inayafanyia kazi ili kuhakikisha kunakuwa na
mabadiliko ya haraka na yenye nguvu na kuifanya Zanzibar kuinuka
kiuchumi.
Alisema ofisi hiyo iliyopewa mamlaka ya kuratibu uwajibikaji wa Taasisi
zote za SMZ zilizopo mjini Dar es Salaam hivi sasa itakuwa chini ya
ofisi Makamu wa Pili wa Rais jambo ambalo litazifanya shughuli za idara
hizo kufanya kazi zake kwa ufanisi.
Alisema serikali iliamua kuanzisha ofisi hiyo mwaka 1986 ili iwe kiunganishi cha upatikanaji wa huduma za kiuchumi kwa urahisi.
Comments