KIRAKA wa Tanzania, Shomari Kapombe
ametambulishwa juzi Ahamisi kwenye mazoezi ya klabu ya AS Cannes ya
Ufaransa, lakini Kocha Mfaransa aliyetimuliwa Simba, Patrick Liewig
amesema timu hiyo haina hadhi ya Kapombe.
Hata hivyo, Simba imemjibu Liewig kuwa asiwe na wasiwasi kwani tayari Kapombe anatakiwa na timu ya daraja la pili ya Ufaransa.
Liewig aliiambia Mwanaspoti kwa simu
kutoka jijini Paris, Ufaransa jana Ijumaa kwamba klabu hiyo ya daraja la
nne ni ya hadhi ya chini sana kulinganisha na ubora wa Kapombe ambaye
alipaswa kuchezea madaraja ya juu hivyo Simba imempeleka sehemu
anakokwenda kupoteza muda wake.
Liewig alisema; "Naijua Cannes ni timu
ndogo sana, inashiriki daraja la nne ni ya chini sana kulinganisha na
ubora wa Kapombe niliyemfundisha hapo Simba. Yeye hadhi yake ni daraja
la kwanza au la pili, na zipo klabu nyingi tu ambazo angeweza kupata
nafasi."
"Simba na huyo wakala wanampotezea
Kapombe muda wake, wachezaji wakubwa wa Tanzania wanapaswa kukaa chini
na kujipanga. Klabu zikae na watu wa maana zifanye mambo kwa kufuata
weledi, mimi najuana na watu wengi sana kuanzia makocha na viongozi
ambao naweza kuwaunganishia wachezaji wa Tanzania na wakacheza soka
daraja la kwanza.
"Mchezaji mwenyewe ajipange anifuate
aonyeshe nia ya kweli mimi nitashirikiana na viongozi nitamsaidia,
lakini huko alikokwenda Kapombe sijapaafiki," alisisitiza kocha huyo
ambaye bado hajapata dili mpya.
Katika klabu hiyo, Kapombe atajumuika na 'Waswahili' wanne kutoka Burundi, Uganda, Senegal na Togo.
Kapombe atakuwa katika klabu hiyo na iwapo atauzwa ndio Simba itapata mgawo wake.
Kapombe atakuwa katika klabu hiyo na iwapo atauzwa ndio Simba itapata mgawo wake.
Hata hivyo, Mwenyekiti wa Usajili wa
Simba, Zacharia Hanspoppe aliliambia Mwanaspoti jana Ijumaa kuwa hawana
wasiwasi na suala hilo kwani tayari Kapombe ameivutia timu ya daraja la
pili.
"Sisi tunajiamini na mambo
tunayoyafanya, hapo nazungumza na wewe nilikuwa napata mawasiliano
kutoka Ufaransa kuwa kuna timu ya daraja la pili inamhitaji Kapombe. Hao
AS Cannes wakimuuza Kapombe sisi tunapata asilimia 40," alisema
Hanspoppe. Chanzo: mwanaspoti
Comments