Wagombea wa kiti cha urais nchini Mali wamesema wana matumaini ya
kushinda duru hiyo ya pili ya uchaguzi wa rais huku kampeni zake
zikikamilika Ijumaa ya jana.
Ibrahim Boubacar Keita Waziri Mkuu wa zamani wa Mali aliypata karibu
asilimia 40 ya kura zilizopigwa na Soumaila Cisse Waziri wa zamani wa
Mambo ya Nje wa nchi hiyo alipepata asilimia 19.4 katika duru ya kwanza
ya uchaguzi huo watachuana tena katika duru ya pili ya uchaguzi wa rais
wa Mali uliopangwa kufanyika kesho Jumapili, baada ya mahasimu hao
kushindwa kupata kura zinazohitajika katika duru ya kwanza.
Keita ambaye alimshinda Cisse kwa zaidi ya asilimia 20 katika duru ya
kwanza ya uchaguzi wa rais amesema ana matumaini ya kushinda uchaguzi wa
kesho kwa kuzingatia matokeo hayo ya hapo awali.
Ibrahim Boubacar Keita ameongeza kuwa, kipaumbele chake cha kwanza
kitakuwa ni mapatano ya kitaifa baada ya nchi hiyo kukumbuwa na mgogoro
na kwamba mwanzo mpya unahitajika huko Mali.
Naye Soumaila Cisse amesema kuwa ana matumaini ya kushinda duru ya pili
ya uchaguzi wa rais hapo kesho akisema kuwa na hapa ninamnukuu" uchaguzi
wa kesho si suala la kuongezea kura zilizopatikana katika duru ya
kwanza, bali ni kuwa kutakuwa na kura mpya na kwamba huo ni uchaguzi
mpya," mwisho wa kumnukuu.Inatoka kwa mdau.
Comments