Dar es Salaam. Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh
Ponda Issa Ponda amesema alichanganyikiwa kiasi cha kushindwa kujielewa
kwa muda baada ya kupigwa risasi.
Akizungumza katika mahojiano maalumu na Mwananchi kwenye wodi binafsi ya
Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (Moi) alikolazwa jana, Sheikh Ponda
alisema kutokana na hali hiyo hakumbuki matukio yaliyofuata baada ya
hapo.
“Sikumbuki hata nilipata huduma ya kwanza hospitali gani kwa sababu
sikuwa katika hali ya kawaida. Mambo mengine yaliyotendeka kabla ya
kujeruhiwa ninayakumbuka vizuri,” alisema Ponda ambaye inasadikiwa
kwamba alipigwa risasi ya begani, Ijumaa iliyopita mjini Morogoro.
Alisema alihutubia katika Kongamano la Waislamu kwa muda mfupi
akizingatia muda uliokuwa umetolewa kumaliza mkutano huo na baada ya
hapo alishuka na kupanda kwenye gari binafsi ambalo lilizingirwa na
polisi ndipo akaamua kushuka na kuanza kutembea kabla ya kujeruhiwa.
Mahojiano maalumu na Sheikh Ponda
Swali: Je, watu waliokupa huduma ya kwanza mara baada ya kujeruhiwa walikuta risasi iliyokujeruhi?
Jibu: Nilipigwa risasi kwa nyuma ikatokea mbele kwa hiyo haikubaki
mwilini wala haikuonekana ilipoangukia kwa wakati huo maana kulikuwa na
purukushani.
Swali: Ulipata wapi huduma ya kwanza?
Comments