Skip to main content

MECHI YA YANGA, ASHANTI YAINGIZA MIL 102/-

ashanti_f0a9e.jpg
Release No. 141
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Agosti 25, 2013
MECHI YA YANGA, ASHANTI YAINGIZA MIL 102/-
Mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Yanga na Ashanti United iliyochezwa jana (Agosti 24 mwaka huu) katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 102,856,000.
Watazamaji 17,744 walikata tiketi kushuhudia mecchi hiyo namba moja ya VPL msimu wa 2013/2014 iliyomalizika kwa mabingwa watetezi Yanga kuibuka na ushindi mnono wa mabao 5-1.

Comments