Maelfu ya watu walikusanyika katika miji
miwili mikubwa nchini Libya,yaTripoli na Benghazi
Ijumaa(15.02.2013)kusherehekea miaka miwili tangu kuanza kwa mapinduzi
yaliyosababisha kuangushwa kwa Moammar Gaddafi.
Katikati ya jiji la Tripoli, mamia yawatu walikusanyika katika
uwanja wa mashahidi , wakipepea bendera na maputo na kuimba
nyimbo za kusifu mashahidi waliokufa katika mapinduzi ya Libya
wakati magari yakipita mjini wakipiga honi.
Mjini Benghazi, mji wa mashariki ambako ulianzia uasi , maelfu
yawatu waliandamana katika njia ile ileya maandamano yaliyofanyika
Februari 15 , mwaka 2012, kichocheo ambacho kilizusha vuguvugu la
mapinduzi siku mbili baadaye.
Waandamanaji Benghazi
Waandamanaji wa Benghazi pia waliwasifu mashahidi , pamoja na wale
ambao wamepotea na wale ambao wamejeruhiwa katika mzozo ambao
ulidumu kwa zaidi ya miezi minane hadi pale alipouwawa kanali
Gaddafi Oktoba 20, mwaka 2011. Lakini waandamanaji pia wamekosoa
viongozi wapya, wakidai hususan kugawana zaidi madaraka.
Serikali tayari imechukua hatua madhubuti za kudhibiti jaribio
lolote la waungaji mkono wa utawala wazamani kufanya fujo huku
waandamanaji wakiwa na hasira wanawashutumu watawala wapya kwa
kushindwa kuleta mabadiliko.
Comments