Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta |
WAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, amewata wakuu
wa mikoa nchini kuondoa woga na kusimama kidete, ili kukomesha vurugu
zinazoendelea nchini yakiwemo mauaji yanayotokana na imani za kidini.
Sitta ambaye pia ni Mbunge wa Urambo Mashariki alitoa kauli hiyo jana
wakati akifungua mkutano mkuu wa mwaka wa Chama Cha Wanasheria wa
Tanganyika (TLS) katika ukumbi wa Chuo cha Mipango mjini Dodoma.
Alisema kama wakuu wa mikoa hawatatimiza wajibu wao, migogoro na
visingizio vya imani za kidini vitaendelea kukithiri siku hadi siku.
Waziri huyo alisema amekuwa akishangazwa na hatua ya viongozi wa mikoa
kushindwa kuzima maasi hayo mapema licha ya kuwa na vyombo muhimu
vinavyowapa taarifa za haraka.
“Wakati mwingine ni uoga wa viongozi wetu, ama kwa kutokujiamini maana
jambo linaaza kwao na wao wanakuwa na mamlaka zote lakini wanashindwa
kuchukua hatua mapema hadi Waziri Mkuu au Rais aingilie kati, hii ni
aibu kweli,” alisema Sitta.
Waziri huyo aliwataka viongozi wa mikoa kujenga ujasiri na kuwa wepesi wa kukabili matatizo yanapotokea katika maeneo yao ili yasilete madhara makubwa katika jamii. Kuhusu wanasheria, alisema licha ya Tanzania kuwa na chuo kikongwe cha kisheria, lakini bado ina upungufu mkubwa wa wanasheria ikilinganishwa na nchi kama Kenya ambayo wanasheria wake walianzia kusoma Tanzania.

Alisema kwa sasa watu waliosajiliwa kama wanasheria nchini Tanzania ni 3500 wakati nchi kama Kenya imesajili wanasheria 11,000.
Comments