Na Harbi Abdillahi Omar, Djibouti
Vyama vya siasa vya Djibouti vilizindua kampeni zao wiki iliyopita
kuelekea uchaguzi wa wabunge tarehe 22 Februari, lakini vyama vya
upinzani vimelalamika kuwa serikali inawazuia fursa zao isivyo halali.
Wafuasi wa Chama cha Union for National
Salvation wakiwa wamekusanyika katika mtaa Avenue 26 wa Jiji la Djibouti
kwa ajili ya mkutano wa tarehe 10 Februari. [Picha ya Harbi Abdillahi
Omar/Sabahi]
Katika kipindi cha wiki mbili zijazo, chama tawala cha Union for a
Presidential Majority (UMP), ambacho kimekuwepo madarakani kwa muongo
mzima, Chama cha upinzani cha Union for National salvation (USN) na
mrengo wa kati cha Centre for Unified Democrats (CDU) vitawasilisha
ajenda zao za kisiasa kwa wananchi. Zaidi ya raia 173,900 wameandikishwa
kupiga kura katika uchaguzi huo.
"Kambi mbili hazishindani katika uwanja sawa wa mchezo," alisema Hamdi
Farah, mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Djibouti ambaye anaunga mkono
chama cha Republican Alliance for Development, ambacho ni sehemu ya
muungano wa vyama vya upinzani. "Kwa kampeni hii, upinzani umeanza na
mwanzo mbaya, kwa vile tovuti zao kadhaa za intaneti bado zinadhibitiwa
na serikali."
Tovuti za upinzani ambazo haziwezi kuonekana kutoka Djibouti ni pamoja
na msemaji wa USN Daher Ahmed Farah wa chama cha Movement for Democratic
Renewal, ambayo inaweza kufikiwa kupitia tovuti ya Waandishi wa Habari
Wasio na Mipaka, Chama cha Republican Alliance for Development na Sauti
ya Djibouti, tovuti mpya ya habari yenye uhusiano na upinzani.
"Upinzani kamwe haukuwahipo kuhakikishiwa kuwa udhibiti wa habari ungeondoshwa," aliiambia Sabahi.
Comments