Boniface Bosire alichangia katika habari hii kutoka Nairobi
Waraka uliotolewa tarehe 18 Februari na Wandishi asiyejulikana akidai
ana mahusiano na al-Shabaab ni ushahidi zaidi kwamba saga linaloendelea
kumhusu mwanamgambo mzaliwa wa Marekani Omar Hammami ni tishio baya --
kama sio hatari -- kwa uongozi wa al-Shabaab.
Waraka mpya wenye ukurasa 17 ndio jaribio
pana zaidi la al-Shabaab kumkataa na kumtenga mwanajihadi mzaliwa wa
Marekani Omar Hammami. [Jalada]
Waraka huo wa ukurasa 17 wenye kicha cha habari "Kukimbia ukweli
hakuwezi kulifanya litoweke: Kufisha hadithi ya Abu Mansour", ni jaribio
pana la kuwaaibisha na kuwatenga wafuasi wa Hammami, anayejulikana pia
kama Abu Mansour al-Amriki, kwa kushambulia utu wake, inia na dhamira
yake katika jihadi.
"Wakati na fedha vinatumiwa kupunguza hasara ambayo tayari imeshafanyika
na mpasuko uliopo [miongoni mwa al-Shabaab]," alisema Samson Omusula,
mshauri wa masuala ya usalama aliyeko Nairobi, na kuongeza kuwa kikundi
cha wanamgambo hakipotezi juhudi yoyote katika kufikia umma wa wasomaji
ulioenea.
"[Waraka huu] ni jaribio [la la-Shabaab] kujionyesha wenyewe kama
kikundi chenye wasiwasi na matatizo ya kifedha na wafuasi ambao
hawakuungana," aliiambia Sabahi.
Masuala madogo yanayojulikana kuhusu mtu anayedaiwa kuandika huu waraka, Abu Hamza al-Muhajir, kuliko kile kilichomo ndani yake.
Waraka huu, ambao umeandikwa kwa Kiingereza cha mitaani na kutolewa na
picha za kuvutia, nukuu za kuvuta, mfumo rahisi wa kidijitali,
unamwonyesha mwandishi kama mtu wa Magharibi katika juhudi za
kuwashawishi wasomaji kwamba yeye na wapiganaji wengine wa kigeni hawako
pamoja na kutoridhika kwa al-Amriki kwa Uongozi wa al-Shabaab.
Hata hivyo, ushahidi unaonyesha uwezekano mkubwa kwamba kwa kweli al-Muhajir ni mwanachama wa Somalia wa al-Shabaab.
Comments